Brazaj, nguvu ya Umma (People's power) isikilizie mbali! Kumbe binadamu ni kiumbe hatari na cha kutisha akiamua kubadilika.Goli la mkono walijua kweli ndugu? Unadhani Mbowe kushindwa Hai walikuwa wadhoofu huko kuliko Nkasi?
Brazaj, nguvu ya Umma (People's power) isikilizie mbali! Kumbe binadamu ni kiumbe hatari na cha kutisha akiamua kubadilika.
Sijui Hai ilikuwaje, lakini, kama scenario ingekuwa kama ya Nkasi, Hai pangewaka moto. Mahali askari na wajeda wanainua mikono ni situation ya mzaha hiyo?
Unakumbuka ya (Tunisia/Algeria?) yule kijana baada ya kujiteketeza moto wa petroli?
Ogopa sana 'people's power'!
Sidhani kwamba tumetofautiana na wala sio swala la kuwaachia nchi CCM. Lilikuwa ni swala la kutofahamiana lugha ingawa sote tunazungumza na kuandika Kiswahili.Habari ndiyo hiyo.
Zawadini kutofautiana kwenye agenda za kina Mwaipopo na wenziwe kusitufanye kuitelekeza nchi kwa ma CCM.
Aliimba mwuungwana, hata watoto mapacha hutokea wakati wakaacha kuelewana. Sembuse miye na wewe ndugu yangu?
Huoni kuwasusia nchi kwa sababu ya ila za Hapa na pale, itakuwa ni afadhali ya kuwasusia fisi bucha ndugu yangu?
Sidhani kwamba tumetofautiana na wala sio swala la kuwaachia nchi CCM. Lilikuwa ni swala la kutofahamiana lugha ingawa sote tunazungumza na kuandika Kiswahili.
Hili la nchi kuwaachia CCM mimi nangojea akina mdude waongoze maandamano baada ya ule muda walouwka wa siku 30 kumalizika. Hivyo ndivyo nilivyoahidi kwamba tutashiriki pamoja iwapo tu yeye mwenyewe atashiriki.
Ninavyofahamu Watanganyika ni waoga naye hatoshiriki. Ukiangalia comment yangu kwenye ule uzi, nilishauri wapate ushauri kutoka kule upande wa pili kwani wao wanao uzoefu wa kutosha, ila wajitayarishe na matokeo ya hayo..
Wasiwasi wangu, hili hawatolifanya kwani wao ni WAOGA.
Sawa nipo nangojea, Mungu akipenda.Hii vita haihitaji kusubiriana. Wakati Mdude anaandaa kuni, hakusimamiahi wengine kuandaa nyanya, mdarasini, pilipili hoho, karoti, au wengine kwenda kuleta chumvi au mafuta ya alizeti.
Hapa umenena!Watanganyika si waoga ndugu yangu. Kujiridhisha tambua tulili himili vilivyo lile jiwe lenyewe kutokea Chatto.
Mkuu nimekaa mkao wa kulaKwa vile unasibiri wewe kaa tuli, kwa kutulia ila kitanuka hapa. Dkt. Slaa anao uzoefu sana kwenye harakati ndume hizi.
Huku huwa tunasubiri filimbi tu. Nadhani una habari na taarifa zake. Historia ni shahidi. Tatizo letu ni kutoka Tanganyika kuingilia kati kwa hofu ya uongo aliyoielezea Lukuvi. Wakituachia mambo yetu kitajulikana.Hayo pembeni, makwetu twaitisha kurejea ubaoni, Nini maoni yenu? Vipi kuhusiana na ACT huko mwajiona je wenzetu? Nchi mwachukua au nanyi mmejipanga kulia lia kama ilivyo ada?
Sawa nipo nangojea, Mungu akipenda.
Hapa umenena!
Mkuu nimekaa mkao wa kula
Huku huwa tunasubiri filimbi tu. Nadhani una habari na taarifa zake. Historia ni shahidi. Tatizo letu ni kutoka Tanganyika kuingilia kati kwa hofu ya uongo aliyoielezea Lukuvi. Wakituachia mambo yetu kitajulikana.