mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
"Wapiga kura waliopiga kura halali za wabunge kwa mujibu wa taarifa ya tume ya uchaguzi walikuwa takribani milioni 11. 8 lakini ukienda kwenye matokeo ya uchaguzi ya kila jimbo katika nchi yetu, ambayo tume iliyachapisha tarehe 5 Januari 2021 ukajumlisha matokeo ya kura halali katika majimbo yote ya nchi hii unagundua kwamba wapigakura halali waliopiga kura za wabunge katika uchaguzi mkuu uliopita ni takribani milioni 8.8, kuna kura zaidi ya milioni 2.1 ambazo hazijulikani zilitokea wapi, na asilimia 92 ya kura hizo zilipelekwa kwa wabunge wa CCM, sisi CHADEMA tumegawiwa hizo kura haramu 148000 lakini kura zaidi ya milioni 2 zilipelekwa kwa CCM, kura haramu kabisa.
Sasa haya yanawezekana kwasababu tume haiwajibiki kueleza mtu yeyote idadi halisi ya wapigakura iliyowaandikisha, tume haiwajibiki kufungua server zake huko wanapohifadhi takwimu za wapiga kura kwa mtu yeyote.
Na kwasababu haiwajibiki kufungua server zake kuonesha hizo takwimu, Tume imekuwa pamoja na serikali na CCM wanatumia mianya hiyo kuingiza mamilioni ya kura feki katika kila uchaguzi, sasa kura feki ni jambo la kawaida"