Kuna mjadala unaendelea na nimeonelea ni vema kuanzisha mwingine ambao itaenda sambamba (baadae kuunganishwa) nikiambatanisha Audio version ya alichokiongea Mzee Malecela tarehe 25 Machi 2009. Hapa ni JamiiForums Listening Audio Booth (J-LAB)
Sikiliza kwa kubonyeza alama ya kucheza moja kwa moja:
[mp3]http://www.jambovideos.com/mahojiano/JM_PC_March.mp3[/mp3]
...He needs to retire from politics..wakati wake umepita!!
Kwa hakika nitamjibu!
Wakuu, Malecela anazungumza kama makamu mwenyekiti wa CCM, ni muhimu sisi tuifahamu lugha yake kwanza...Huyu sii kiongozi wa serikali na hana nguvu huko..
Pili, alichosema ni ukweli mtupu.. kwani kama kweli hawa jamaa wanaotaka kumeguka CCM watoke! hizi habari za kutuzuga hata sisai wananchi hatufahamu wanachosimamia ni kutuzidishia hasira tu.. Waondoke CCM, wananchi tujue moja kama ni hao Mafisadi wanatishia kuondoka waondoke.. na kama kuna wale wanaojiona wasafi na CCM sio mahala pao - waondoke...
Jamani ndilo sisi wananchi tunachotaka kuona na tunatarajia mtu yeyote mwenye kujali maslahi ya Taifa atakuwa amechukua maamuzi ya maana isipokuwa wale wanaotaka kutubeza..sio kuitisha vikao kila siku kujitangaza wajkati bado wamo ndani ya chungu wakipikwa..
Wakuu, Malecela anazungumza kama makamu mwenyekiti wa CCM,