Lita moja ya mafuta imefika 2,200, serikali ipo wapi?

katika sh 2200 kodi ni sh 1400 inakula serikali na taasisi zake!
 
busara basi! Unajua kodi kwa lita ni sh ngapi? Mbona landlocked countries jirani na sisi bei chini?
Kipo chanzo kimoja cha habari kilisema kila lita moja ya mafuta kodi ya Serikali ni 540/=wadau wenye habari zaidi tusaidieni ili tupate majibu kwa usawa
 
Kipo chanzo kimoja cha habari kilisema kila lita moja ya mafuta kodi ya Serikali ni 540/=wadau wenye habari zaidi tusaidieni ili tupate majibu kwa usawa

Yan kibaya zaidi hizi kodi ndo zinampeleka kikwete ulaya kila kukicha!kheri zingekua zinafanya kazi ya maana kdg mtu ungeelewa!
 

Well said kaka!
 

Upo wap muheshimiwa?halaf me kinachonishangaza mafuta ya nchi jiran yanapita kwetu na extra cost za usafirishaji bado yanauzwa bei ya kawaida kwao,huu mfumuko kwetu unatokana na nini?
 
Kenya imekuwa rahisi si kwa vile wana viongozi bora la hasha wana wananchi wenye msimamo na wasiodanganyika, wale kubeba mapanga na kumgeuza mtu bucha ni kitendo cha sekunde. Na mgomo wao ule ungeelekea kumtoa presdaa wao madarakani akasoma alama za nyakati na akakumbuka lile timbwili la 2008 akashusha bei haraka. Hapa kwetu ni ngumu wananchi sisi tu waoga sana tukiandamana kikija kifaru tunazimia wote wengine wanaachia mpaka hewa chafu shauri ya woga wa kirungu na maji ya kuwasha. Hii nchi labda tuzaliane kwa wingi na waarabu tuondoe hii damu ya kimdebwedo.
 

Imeshuka kwa 10% lakini EWURA hawana habari, Ila ikipanda tu, utawasikia wanapandisha bei!
 
wewe unajua bei ya mafuta kitika soko la dunia? au ndio kuropoka, kama mafuta yamepanda bei kwa wanaochimba je unategemea nini kwa nchi kama Tanzania.
Sio lazima kujibu kila hoja kwa utetezi bila kuwa na uhakika na kile unachoandika. Au posho yako nikwa kila post unayo weka napa jamvini?
 

Unatumia gari gani? ishi kwa wakati mwenzio mie nina ka cororola haka lita kumi siku tatu! tatizo mnajitutumua na madude makubwa alafu unalia mafuta. Uza gari lako na nunua Bajaji chupa ya soda utapiga misele wiki moja. Upo hapo! hacha kulia ndo hali halisi nenda mashariki au magharibi. Kwanza badilika mwenyewe mpaka tutakapo anza chimba mafuta yetu ndo mnunue hayo ma VOGUE!
 
Think BIG, kwani kuna hivi karibuni umesikia serikali imeongoza kodi kwenye mafuta? The rest serikali ya Tanzania haimiliki visima vya mafuta....

Hivi mtu ukiwa ccm hata uwezo wa kupambanua mambo unayeyuka?
 
Hukukosea kujiita Nguli Jabali, mpaka mambo ya hewa chafu yote included, duuuuuh kisa woga. Ngoja CDM watishe maandamano, utasikia JK akilalama kama vile haoni.
 
Serikali isipokuwa makini na huu mfumuko wa mafuta itashindwa hata kujiendesha maana hata budget zilizopitishwa zitapitwa na wakati baada ya muda kidogo.
 
Kupunguza kodi ya mafuta ya taa na diesel kenya,kutawapunguziaje inflation?...naomba elimu,kwa sababu hii naona kama imekaa kiunazi unazi vile!
 
yani naumia sana kwa hii hali ila Mungu atatusaidia muda siyo mrefu kwa nini chadema wasiandamane kupinga kwa ongezeko la bei ya mafuta waone jins watu watakavyo waunga mkono kwa sababu ndicho kitu kkinacho watesa watu
 
NITAUKUMBUKA NA KUUENZI......."UJAMAA" siasa thabiti kwa nchi zinazoendelea
 
Imeshuka kwa 10% lakini EWURA hawana habari, Ila ikipanda tu, utawasikia wanapandisha bei!

je EWURA wanakula na wamiliki wa vituo vya mafuta? 10% ? bei ya mafuta kwenye soko la dunia ilishashuka na hii ni kweli tena imeshuka kwahiyo hiyo kumi
 

nimekusoma mukuluuu
 
wewe unajua bei ya mafuta kitika soko la dunia? au ndio kuropoka, kama mafuta yamepanda bei kwa wanaochimba je unategemea nini kwa nchi kama Tanzania.

Hujamtendea haki muanzisha thread hii. Unaposema anaropoka una maana gani? Mbona wewe ndiye unayeonekana unaropoka? Anauliza iwapo trend hii ya kupanda kwa bei ya mafuta inaweza kuwa arrested. Anataka kujua kama serikali inaweza kufanya lolote kupunguza makali yanayosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta. Tunatarajia kama great thinkers yatolewe majibu ya kisomi. Hebu tuwasubiri watu wenye hoja waje watuelimishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…