Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Shikamooni wanaJamiiForum wote.
Leo napenda kuwaletea historia ya huyu mwanamama anayeitwa Letti Kidanka sijui ni jina lake halisi au
Alikuwa mchawi maarufu sana na pia mtawala huko maeneo ya mkoa wa Singida.
Sifa kubwa aliyokuwa nayo huyu mama ni kupambana vita na wajerumani miaka ya 1891 kama sikosei.
Silaha yake kubwa alikuwa anatumia nyuki kuwafurusha wajerumani
=====
Michango ya Wanachama...
Leo napenda kuwaletea historia ya huyu mwanamama anayeitwa Letti Kidanka sijui ni jina lake halisi au
Alikuwa mchawi maarufu sana na pia mtawala huko maeneo ya mkoa wa Singida.
Sifa kubwa aliyokuwa nayo huyu mama ni kupambana vita na wajerumani miaka ya 1891 kama sikosei.
Silaha yake kubwa alikuwa anatumia nyuki kuwafurusha wajerumani
=====
Michango ya Wanachama...
Kwa hisani ya mdau toka Singida:
Leti (au Letti kama ulivyomtambulisha kwetu) Kidanka anadaiwa kuwa aliitangaza Tanzania ktk kila pembe ya Dunia kwa Ushindi wa kutumia zana za Asili dhidi ya Wajerunabu. Nakumbuka niliwahi kuongea na aliyekuwa Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo, Bi. Anna Mghwira akaniambia ni mmoja wa watu waliompa hamasa ya kujiingiza kwenye siasa.
-> Anadaiwa kuwa alipambana na kuwashida Wajerumani zaidi ya Mara 3.
SIMULIZI LENYEWE:
Leti Kidanka ni Mwanamke shujaa aliyewaongoza kabila la Wanyaturu katika mapambano dhidi ya utawala wa kijerumani.
Kwa mujibu wa familia iliyopo, Leti alizaliwa katika kijiji cha Unyang’ombe – Sekotoure Ilongero. Aliolewa na Nyalandu Mtinangi wa Ukoo wa Lundi (Antuamwa Lundi) katika kijiji cha Matumbo Kitongoji Mikuyu, Kata ya Makuro wilayani Singida vijijini..
Wazazi wake walikuwa waganga wa tiba asilia Kidanka Jilu Msasu na Sita Mughenyi, Leti naye alirithi uganga huo toka kwa wazazi wake. Wengi walidhani alikuwa mchawi!
Ushujaa wake ulijitokeza zaidi katika ukoo mdogo wa Lundi alikoolewa wakati alipowatumia nyuki kama silaha ya kudhoofisha nguvu za maadui wake na kuwasambaratisha walipojaribu kumkaribia.
Maadui wake wakuu, walikuwa ni wakoloni wa Kijerumani wakishirikiana na vibaraka wao wa ukoo wa Unyanjoka ukiongozwa na Igwe Yunga kumkabili mwanamama huyo.
Mapambano hayo yalichukua miaka mitatu, kati ya 1908 na 1910. Kibaraka wa wakoloni, Igwe alitafuta nguvu za ziada za kukabiliana na Leti alipolileta jeshi la kijerumani kutoka Kilimatinde wilayani Manyoni, baada ya wao kushindwa.
Katika pambano hilo la mara ya pili kati ya wajerumani Wanyanjoka na kikosi cha Leti, askari wa kijerumani aliyejulikana kwa jina moja la “SAUSI” aliuwawa kwa kuchomwa mkuki na mume wa shujaa huyo, Nyalandu Mtinangi mwaka 1909.
Leti alipambana na maadui hao mara mbili na kuwashinda. Safari ya tatu mnamo mwaka 1910 hakuweza kufanikiwa kuwashinda, badala yake aliuwawa nyumbani kwake pamoja na mume wake katika kijiji cha Matumbo Kitongoji cha Mikuyu Singida vijijini.
Umaarufu wa Leti ulitokana na ujasiri aliokuwa nao akiwa ni mwanamke, kwa kuwatumia nyuki kama silaha yake ya kuwashambulia maadui huku akisaidiwa na wafuasi wake ambao walikuwa ni mume wake Nyalandu na shemeji yake Hango Linja, wakitumia Mikuki na mishale.
Mwanamke huyo aliongoza mapambano yeye mwenyewe kwa kutoa amri kwa washirika wake kushambulia au kusitisha mapigano katika eneo la vita.
=" Mwanamke shujaa aliyewaongoza kabila la Wanyaturu katika mapambano dhidi ya utawala wa kijerumani, si mwingine ila ni Leti Kidanka, katika vita vikuu vya pili vya dunia mwaka 1938 hadi 1945.
Kwa mujibu wa familia iliyopo, Leti alizaliwa katika kijiji cha Unyang’ombe – Sekotoure Ilongero. Aliolewa na Nyalandu Mtinangi wa Ukoo wa Lundi (antuamwa Lundi). Katika kijiji cha Matumbo Kitongoji Mikuyu, Kata ya Makuro wilayani Singida vijijini..
Wazazi wake walikuwa waganga wa tiba asilia Kidanka Jilu Msasu na Sita Mughenyi, Leti naye alirithi uganga huo toka kwa wazazi wake..
..Ushujaa wake ulijitokeza zaidi katika ukoo mdogo wa Lundi alikoolewa. Wakati alipowatumia nyuki kama silaha ya kudhoofisha nguvu za maadui wake na kuwasambaratisha walipojaribu kumkaribia.
Maadui wake wakuu, walikuwa ni wakoloni wa Kijerumani wakishirikiana na vibaraka wao wa ukoo wa Unyanjoka ukiongozwa na Igwe Yunga kumkabili mwanamke huyo.
Mapambano hayo yalichukua miaka mitatu 1908 hadi 1910. Kibaraka Igwe alitafuta nguvu za ziada za kukabiliana na Leti alipolileta jeshi la kijerumani kutoka kilimatinde wilayani Manyoni, baada ya wao kushindwa.
Katika pambano hilo la mara ya pili kati ya wajerumani Wanyanjoka na kikosi cha Leti. Wakati askari wa kijerumani aliyejulikana kwa jina moja la “SAUSI” aliuwawa kwa kuchomwa mkuki na mume wa shujaa huyo Nyalandu Mtinangi mwaka 1909..
Leti alipambana na maadui hao mara mbili na kuwashinda. Safari ya tatu mnamo mwaka 1910 hakuweza kufanikiwa kuwashinda, badala yake aliuwawa nyumbani kwake pamoja na mume wake katika kijiji cha Matumbo Kitongoji cha Mikuyu Singida vijijini.
Umaarufu wa Leti ulitokana na ujasiri aliokuwa nao akiwa ni mwanamke, kwa kuwatumia nyuki kama silaha yake ya kuwashambulia maadui huku akisaidiwa na wafuasi wake ambao walikuwa ni mume wake Nyalandu na shemeji yake Hango Linja, wakitumia Mikuki na mishale,
Mwanamke huyo aliongoza mapambano yeye mwenyewe kwa kutoa amri kwa washirika wake kushambulia au kusitisha mapigano katika eneo la vita.
Salum Chilwa said:"IJUWE HISTORIA YA LETI MWANAMKE WA KINYATURU ALIYEPAMBANA KIVITA WAKATI WA UTAWALA WA KIJERUMANI.
" Ni mwanamke shujaa wa kabila la kinyaturu aliyeongoza Wanyaturu katika mapambano dhidi ya utawala wa kijerumani anaitwa LETI KIDANKA kwa mujibu wa familia take iliyopo wanasema LETI alizaliwa katika kijiji cha unyang'ombe-sekotoure ilongero,aliolewa na NYALANDU MTINANGI wa ukoo wa Lundi(#antuamwa lundi) kutokana kijiji cha matumbo kata ya makuro iliyopo Singida vijijini.
Wazazi wake LETI walikua waganga wa tiba asilia ambao ni KIDANKA JILU MSASU na SITA MUGHENYI,LETI Nate alirithi uganga huo kutokana kwa wazazi wake.ushujaa wake ulianza kuonekana katika ukoo mdogo wa lundi alikoolewa,wakati alipotumia nyuki,mikuki na mishale kudhoofisha maadui zake kila walipomkaribia.
Maadui sake walikuwa ni wajerumani na vibaraka zao wa ukoo wa #unyanjoka ukiongozwa na IGWE YUNGA kumkabili LETI, mapambano hayo yalidumu kwa miaka mitatu,1908-1910 igwe alitafuta nguvu za ziada kukabiliana na LETI alipoleta jeshi la kijerumani kutokana kilimatinde wilayani manyoni baada ya wao kushindwa,katika pambano hilo la Mara ya pili kati ya wajerumani wakishirikiana na wanyanjoka dhidi ya kikosi cha LETI, asikari wa kijerumani aliyejulikana kwa jina moja la "SAUSI" aliuwawa kwa kuchomwa mkuki na mume wa LETI nyalandu mtinangi mwaka 1909 LETI akashinda kwa Mara ya pili.
Mnamo mwaka 1910 leti hakufanikiwa kushinda kutokana na usaliti uliofanywa na mmoja wa washirika wake na kuuwawa pamoja na mume wake katika kijiji cha #matumbo kitongoji cha mkuyu.
Umaarufu wa LETI KIDANKA ulitokana na ujasiri wake kwenye uwanja wa kivita kwa kushirikiana na mume wake pamoja na shemeji yake #Hango_Linja kwa kutumia zaidi nyuki,mikuki na mishale,LETI alishiriki kikamilifu kwa kutoa amri kwa washirika wake kushambulia au kusitisha mapambano.
Pia alijihami kwa kutumia(sumanda)handaki kwa kujificha wasionekane na maadui,hivyo ni baadhi ya vitu vilivyompa umaarufu.
Kushindwa kwake ni pale dawa zake zilipokosa nguvu na hatimae kuuwawa baada ya usaliti uluofanywa na mshirika wake SIE NDIDA make wa shemeji take Hango Linja walioishi eneo moja na kujenga urafiki na adui yao igwe yunga mshirika wa wajerumani uliomfanya kutoa siri ya ushujaa wao.
Side alirudi kwa siri eneo la zindiko na kuhamisha dawa zote upande wake,mwenzake LETI alipojaribu kutumia maadui walizidi kumkaribia hatimae alikutwa nyumbani kwake akiwa amekaa na kupigwa risasi yeye pamoja na mume wake na kufa papo hapo na miili yao ilizikwa baada ya siku tatu kwa kuhofia kurudi kwa adui zao.
Hapo ukawa mwisho wa mapambano, hawakuendelea kwenda kwa #sie msaliti Ukweli huo unadhihirishwa na wimbo wa kinyaturu usemao "sie sie na LETI,asungu atrufu,vikhoma nkingi vasuka vikuranga....(sie na sie na leti wanawake watupu wamezipiga mambo na kuzing'oa wenyewe).
Leti alikuwa na watoto wanne wawili wa kiume na wengine wa kike,kati ya hao watatu mmoja wa kiume aliitwa #sang'ida,wasichana ni nyamughenyi na sita walikamatwa na kuchukuliwa na wajerumani hadi Dar es salaam baada ya wazazi wao kuuwawa,licha ya kuchukua watoto hao walikata kichwa cha leti na kuondoka nacho had I ujerumani.
" Mtoto mwingine aliyeeitwa #kidanka katika kupurukushani alifanikiwa kutoroka huku akiwa na jeraha la risasi ubavuni kwake,naye alitibiwa kienyeji na kupona akaendelea na shughuli zake mpaka akipofariki mwaka 1980 kijijini hapo,mpaka sasa koo hizi mbili Lundi na Unyang'ombe hushirikiana kutambika Mara kwa Mara katika eneo husika kwa nia ya kunusuru majanga yanayoweza kutokea..
Anna Mghwira said:Wanamabadiliko wenzangu,
Ninaamini sisi ni miongoni mwa wengi ulimwenguni wanaopenda kuona ulimwengu huu unakuwa mahali salama pa kuishi, kulea watoto wetu, jamii zetu na mazingira mengine yote ya maisha. ninaamini pia kuwa sisi tunaweza kuwa chimbuko la amani duniani, endapo tutafanikiwa kusimamia misingi ya mabadiliko inayoleta tija. moja ya changamto za maisha wakati huu na karne hii ni mahusiano kati ya wanawake na wanaume, hili ni bomu ambalo lisipoangaliwa nalo linaweza kuwa janga la kitaifa.
Miaka ya shule nilifanya tafiti kuhusu utambulisho wa watoto nikakuta kuwa kumbe ijapokuwa watoto wote - pamaoja na mimi tunafahamika kwa jina la baba zetu, kimsingi utambulisho wa mtoto unatokana na utambulisho wa mama yake: yaani " the status of a child is often determined by the status of its mother..." not by itfather or father blood. so we speak of a child born in or out of wedlock - by its mother...and a child born of a widow - not widower...a child of an educated mother...a poor mother...or a child born of a woman marrying another woman...si lesbianism ila mwanamke aliyetoa mahari...musoma kule nk....angalia historia na anthropology.... kuhusu suala hili, la mwanamke kiongozi wa dini, zipo dini zenye wanwake viongozi wa jamii na dini.
Singida kuna makabila aina mbili matrilieneal na strongly patrilineal. kwa wanyiramba kuwa na kiongozi mwanamke si suala maana ukoo hufuata wajomba na dada zao, warimi - wanyaturu - ni strongly patrilineal, mimi ni mnyaturu...kule kwetu licha ya kuwa strongly patrilineal, tuliwahi kuwa na kiongozi mwanamke mtemi na kiongozi wa dini aliyfanya matambiko na sadaka za kimila. mama huyu alipigana vita vya mjerumani akawashinda wajerumani mwanzoni, alitumia nyuki kuwaua wajerumani waliokuja kuchukua vijana kupigana vita yao - waliyoiita vita ya dunia...Letti alifanikiwa kuwafukuza kwa nguvu zake za kidini na kiutawala. alitengeneza nyuki akawaweka kwenye vibuyu vya maji, adui alipofika vibuyu vilivunjwa nyuki wakatoka wakawauma jamaa wale mpaka kufa...walikufa wengi mpaka wakamtafuta huyo mama mtawala chief - long story ninaifanyia utafiti ambao karibu utakamilika...nitatoa taarifa kamili humu na kitabu chake kiko mbioni... waliposhindwa wajerumani na tabia yao ya rushwa waliwapa ndugu wa karibu rushwa wakataja mahali alipokuwa amejificha Letti, wakamkamata, wakamnyonga boma ya singida - wakachukua kichwa chake kama walivofanya cha mkwawa, habari yake haijaandikwa sana kama ya mkwawa inasemekana waliona kujidhalilisha kupigwa na mwnamke kama tunavyojaribu kufanya leo.
Kwa hiyo hatuijui habari ya mama huyu na wengine wengi zanzibar, kusini mwa tanzania, hata za bibi titi hazifamhamiki kama za nyerere na kawawa...so the maxim that a woman should keep her place in the kitchen remains... sioni tatizo kubadilishana mawazo lakini kuwa na staha katika matumizi ya maneno ni ustaarabu wenye tija. Kitheologia pia ijapokuwa kanisa katoliki linakataa mpaka sasa kuwapa wanawake upadre, ninawajua masista wengi wa kikatoliki ambao wameanza tangu miaka ya 80 kuomba kupewa kibali cha kutoa huduma. mimi pia ni mtheologia wa kilutheri na katika theologia kama taaluma tunafahamiana, tuna vyama vyetu vya kitaaluma ambavyo tunakutana na kuongelea mambo mbalimbali. ninalijua hili na ninajua litatokea maana kama hakuna mtu anaweza kumkataza mwanamke kuoana na mwanamke mwingine kama mume wa ndoa si bora akawa padre pia?? ama lipi bora kuwa shofa na msagaji ama kuwa padre wa kanisa.
Kama kuwa mwalimu na mwelekezi. zaidi ya yote sisi pia tumepata vikwazo vingi katika wito huu, hata ilifika mahalai unakatazwa kusema una wito kwa jinsi hoja zinavyotoka na kukuandama. hata hivyo aliyekuwa kipofu na akaona utamfanyaje aseme haoni?? nalikuwa mtoto na sasa ni hivi na sijamwona anayeweza kutamka vinginevyo. na katka kazi hiz za wito suala si kazi , sula ni huduma tu ...kianzia shemasi, katekist, mpka pope wote ni wahudumu kama kridto alivyokuwa mtumishi wa kanisa si bwana wa kanisa...paulo na wengien wote pia. indeed upope na uchungaji nk ni taratibu za kibinadamu kuweka mipaka kwa mambo mbalimbali, mengi ambayo tunafunuliwa kila kukicha.
Tunajifunza kila siku mpaka mwisho wa maisha... na kuhusu suala la kichwa cha nyumba, tusemeje juu ya familia zinazolelewa na mama tu?? na bibi tu au shangazi ambazo kwa sasa ni nyingi kuliko zenye bahati ya kuwa na kichwa baba? mungu wa amani na atupe kutambua na haya....
Anna
Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Mh. Harrison Mwakyembe, alisema Wizara yake inaewndelea na utaratibu wa kuyaorodhesha maeneo yote ya kihistoria kwa ajili ya kuyahifadhi na kuyakarabati kwa ajili faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Aidha Waziri huyo alisema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni Muswada wa Sheria ambayo utafanya maeneo ya kihistoria yasiguswe na kuzuia uharibifu.
Alisema baada ya muswada huo kupitishwa na hatimaye kuwa Sheria utasaidia kulinda utajiri wa urithi wa Kihistoria ulipo hapa nchini usiweze kuharibiwa na kupotea.
Katika hatua nyingine Mwakyembe alisema Serikali itahakikisha inarudisha nchini Fuvu la Kichwa cha Mama Shujaa mpiga ukoloni wa Kijerumani kutoka Singida Bibi Liti.
Alisema Shujaa huyo aliweze kupambana na Wajerumani kwa kutumia nyuki hadi hapo aliposalitiwa na wenzake na hatimaye Wajerumani wakata kichwa chake na kuondoka nacho.
Mwakyembe alisema lazima fuvu la kichwa lirudishwe nchini na kuhifadhiwa katika jumba maalumu kwa ajili ya historia ya Tanzania