Liti Lerti Kidanka: Mwanamama toka Singida aliyetumia nyuki kupambana na Wajerumani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Shikamooni wanaJamiiForum wote.


Leo napenda kuwaletea historia ya huyu mwanamama anayeitwa Letti Kidanka sijui ni jina lake halisi au

Alikuwa mchawi maarufu sana na pia mtawala huko maeneo ya mkoa wa Singida.

Sifa kubwa aliyokuwa nayo huyu mama ni kupambana vita na wajerumani miaka ya 1891 kama sikosei.

Silaha yake kubwa alikuwa anatumia nyuki kuwafurusha wajerumani

=====

Michango ya Wanachama...





 
Kwa hisani ya mdau toka Singida:

Leti (au Letti kama ulivyomtambulisha kwetu) Kidanka anadaiwa kuwa aliitangaza Tanzania ktk kila pembe ya Dunia kwa Ushindi wa kutumia zana za Asili dhidi ya Wajerunabu. Nakumbuka niliwahi kuongea na aliyekuwa Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo, Bi. Anna Mghwira akaniambia ni mmoja wa watu waliompa hamasa ya kujiingiza kwenye siasa.

-> Anadaiwa kuwa alipambana na kuwashida Wajerumani zaidi ya Mara 3.

SIMULIZI LENYEWE:

Leti Kidanka ni Mwanamke shujaa aliyewaongoza kabila la Wanyaturu katika mapambano dhidi ya utawala wa kijerumani.

Kwa mujibu wa familia iliyopo, Leti alizaliwa katika kijiji cha Unyang’ombe – Sekotoure Ilongero. Aliolewa na Nyalandu Mtinangi wa Ukoo wa Lundi (Antuamwa Lundi) katika kijiji cha Matumbo Kitongoji Mikuyu, Kata ya Makuro wilayani Singida vijijini..

Wazazi wake walikuwa waganga wa tiba asilia Kidanka Jilu Msasu na Sita Mughenyi, Leti naye alirithi uganga huo toka kwa wazazi wake. Wengi walidhani alikuwa mchawi!

Ushujaa wake ulijitokeza zaidi katika ukoo mdogo wa Lundi alikoolewa wakati alipowatumia nyuki kama silaha ya kudhoofisha nguvu za maadui wake na kuwasambaratisha walipojaribu kumkaribia.

Maadui wake wakuu, walikuwa ni wakoloni wa Kijerumani wakishirikiana na vibaraka wao wa ukoo wa Unyanjoka ukiongozwa na Igwe Yunga kumkabili mwanamama huyo.

Mapambano hayo yalichukua miaka mitatu, kati ya 1908 na 1910. Kibaraka wa wakoloni, Igwe alitafuta nguvu za ziada za kukabiliana na Leti alipolileta jeshi la kijerumani kutoka Kilimatinde wilayani Manyoni, baada ya wao kushindwa.

Katika pambano hilo la mara ya pili kati ya wajerumani Wanyanjoka na kikosi cha Leti, askari wa kijerumani aliyejulikana kwa jina moja la “SAUSI” aliuwawa kwa kuchomwa mkuki na mume wa shujaa huyo, Nyalandu Mtinangi mwaka 1909.

Leti alipambana na maadui hao mara mbili na kuwashinda. Safari ya tatu mnamo mwaka 1910 hakuweza kufanikiwa kuwashinda, badala yake aliuwawa nyumbani kwake pamoja na mume wake katika kijiji cha Matumbo Kitongoji cha Mikuyu Singida vijijini.

Umaarufu wa Leti ulitokana na ujasiri aliokuwa nao akiwa ni mwanamke, kwa kuwatumia nyuki kama silaha yake ya kuwashambulia maadui huku akisaidiwa na wafuasi wake ambao walikuwa ni mume wake Nyalandu na shemeji yake Hango Linja, wakitumia Mikuki na mishale.

Mwanamke huyo aliongoza mapambano yeye mwenyewe kwa kutoa amri kwa washirika wake kushambulia au kusitisha mapigano katika eneo la vita.
 
mohammed said pita huku uongeze historia
 
Kwa bahati mbaya sana historia tuloisoma shuleni hatujafunzwa uwepo wa huyu mama. Natumai wana historia wanaweza kuanza kufukua kilichojiri hapo Singida ili jamii ifahamu uwepo wake
 
Kwa bahati mbaya sana historia tuloisoma shuleni hatujafunzwa uwepo wa huyu mama. Natumai wana historia wanaweza kuanza kufukua kilichojiri hapo Singida ili jamii ifahamu uwepo wake
Yaani ndiyo nimeona leo facebook,ikabidi nimgugo,kila siku nyerere tu,wakati alikunywa mvinyo na wakoloni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…