Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Niko hapa jengo la PSSSF Golden Jubilee Hall, DSM, Wadau Sekta Nguo na Mavazi wa Kitanzania, wamewataka "Watanzania kuvaa, zilizobuniwa na wabunifu wa Kitanzania, na nguo za kushoneza zaidi, na kuvaa ready made za made in Tanzania" badala ya kushobokea nguo kutoka nje ya nchi, cheap imports, huku wenye kipato kidogo, kuishia mtumbani au cheap imports from China!.
Vito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Mzee Kasore wakati wa makaribisho wadau wa sekta ya nguo na mavazi kama sehemu ya maadhimisho ya Miaka 30 ya VETA.
Mgeni rasmi ni Waziri wa Elimu, na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Prof. Adolf Mkenda.
Saa hizi mada zinawasilishwa.
Mada ya kwanza imewasilishwa na Mustapha Hassanali, mbunifu mavazi Mtanzania, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wabunifu Mitindo wa Tanzania (Fashion Designers Association of Tanzania).
Hassanali ameanza kwa kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Mzee Kasore, kwa kuvaa nguo za Tanzania, amewataka Watanzania kuvaa nguo za Tanzania, na hata kama ni kununua nguo, basi wanunue nguo made in Tanzania, ili kuwainua Watanzania.
Amewasisitiza Viongozi kuonyesha mfano wa uzalendo wa kuvaa nguo za Tanzania, kuijenga Tanzania, ukivaa nguo za China, unajenga China, ukivaa nguo za nje, unajenga huko mnakotoka.
Mustafa Hassanali, ambaye ana asili ya Mhindi, amefanya jambo moja kubwa sana la uzalendo, kuliko hata Watanzania wenyewe, ametoa siri, kuwa biashara kubwa kabisa ya nguo, inafanyika mitandaoni. Hayo maduko ya nguo yanayoonekana kutapakaa mahali kwingi, mauuzo ya dukani ni kidogo kuliko mauzo ya mtandaoni, wale wanaofanya biashara kupitia madukani, wana leseni za biashara, hivyo wanalipa kodi, lakini ile biashara ya mitandaoni ambayo ndio biashara kubwa zaidi, hawalipi kodi, na kuna namna yoyote ambayo serikali inaweza kujua na kutoza kodi!.
Biashara inafanyika kwenye simu, whatsapp, instagram, tiktok, na youtube ambayo serikali haina namna yoyote ku monitor na kutoza kodi. Biashara kubwa zaidi, inafanyika majumbani, display ni online kwenye social media, bidhaa zinaonyeshwa pale, na hawaweki bei, unatakiwa kuingia in box unapewa bei, unalipa online, mtu wa boda boda anakuletea mzigo wako, na maisha yanaendelea.
Mustafa Hassanali, amewaomba Watanzania, wengi ni Wakristo na Waislamu na huu ni mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu na Kwaresma, kwa Wakristu, amewaomba wale wote wanaofanya biashara online, wajisajili bure TRA kupatiwa TIN Number, na kupitia TIN number hizo, wajitolee tuu wenyewe kulipa kodi kwa kujitolea, hata ukilipa elfu 5, hata ukilipa elfu kumi, utabarikiwa!.
Karibuni.
Paskali.