Live From Golden Jubilee Hall, DSM, Miaka 30 ya VETA, Kongamano la Wadau Sekta Nguo na Mavazi: "Watanzania Vaeni Nguo za Tanzania" Made in Tanzania!.

Naungana na mdau hapo, tujitahidi kurefine production, hii ifanye bei iwe affordable kwa watu wengi, na hapo watatupata watanzania kwasababu hii ndio hali halisi ya uchumi wetu.
 
Unasemaga muwakilishi wa jamii forums labda kama umebadilisha siku hizi nitakuelewa
Sijawahi kusema mimi ni mwakilishi wa jf, uzuri wangu, kila ninachosema huwa nina kirekodi, ukiniletea clip yangu yoyote, nimesema naiwakilisha jf, ilete, ulamba 10M. leo leo!.
P
 
Waziri Mkenda amesema anataka kuiona VETA ikifanya transformation kuibadili Tanzania, ka ma Tanroad walivyojenga mabarabara nchi nzima. VETA inajenga vyuo nchi nzima, kila mkoa na kila wilaya, vyuo hivi vitumike kama transformation centers.

P
 
amewaomba wale wote wanaofanya biashara online, wajisajili bure TRA kupatiwa TIN Number, na kupitia TIN number hizo, wajitolee tuu wenyewe kulipa kodi kwa kujitolea, hata ukilipa elfu 5, hata ukilipa elfu kumi, utabarikiwa!.
Siku Kodi zikianza kutumika vizuri watu watakua na wito wa kulipa Kodi Kwa Sasa kila mtu ashinde mechi zake
 
Mbona hautuambii hivyo viwanda vya nguo vilipo, mimi ninajua Urafiki, Kilitex, Musoma Tex, Morotex, Sunguratex, Gossage(Tanga) vilikufa, au umevifufua?
 
Waziri Mkenda, amesema anaisema vizuri VETA, ameipongeza VETA, ameipongeza bodi ya VETA na kuipongeza menejimenti ya VETA.

Akawakumbusha, wakipewa maelekezo kutoka juu, ni watekeleze, kama hayatekelezeki, warejee, na sio kutokutekeleza halafu kuanza kuja kufuatiliana na kuulizana.
P
 
Navaa batik sana.
Pia nafundisha kuchoma batik, I'm a SIDO product.
Mamnde, Mamndenyi , mimi ni promota mzuri sana wa wajasiliamali, niite, nikutangazia unachofanya, utauza zaidi na kupata wanafunzi wengi zaidi, tena kama ninavyojitambulisha, mimi ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea, nafanya kazi bure kwa kujitolea.
Hi ni baadhi ya efforts zangu kujitolea humu jf.
 
Hivyo vitambaa vinafumwa na kiwanda gani nchini?
 
Mafundi wengi mitaani wanawashoneaga wamama nguo
Wapo mafundi wazuri wa kushona suti pia za kiume miaka nenda rudi
Ila Pascal Mayalla unaijua bei ya suti ya kushona

Ova
 
Mafundi wengi mitaani wanawashoneaga wamama nguo
Wapo mafundi wazuri wa kushona suti pia za kiume miaka nenda rudi
Ila Pascal Mayalla unaijua bei ya suti ya kushona

Ova
Huwezi amini, nilishona suti mara moja tuu, ndio mara yangu ya kwanza na ya mwisho, nilikuwa nasimamia harusi nililipiwa sikuwahi kujua bei na sijawahi kuuliza!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…