Live from Tunis: Tunisia vs Tanzania

Duuh kweli usimba na uyanga ni tatizo kwakweli, yaani shabiki anakuwa ghafla kocha mmh!
Yaani leo hii unawaza kuwafunga Tunisia kabsaa hahaha duuh, kile kikosi cha Tunisia kilichoanza asilimia 99 ya wachezaji wanacheza nje isipokuwa golikipa. Tuache kuwaza upuuzi ase, wenzetu serikali imewekeza kwenye michezo, wenzetu wachezaji wanalelewa na kukuzwa kwenye academy maalumu, tunashindwa kutoa ushauri kwa serikali badala yake unawaza kumfunga Tunisia aliyekuzidi kila kitu khaaa!! Kufungwa goli moja na ile timu ni jambo la kujisifia na kumpa kongole kocha kwa plan yake, vilevile wachezaji wanapaswa kupewa sifa kwa upambanaji wao. Tuache ushabiki wa kipuuzi na tujikite kwenye kuililia nchi yetu kuwekeza kwenye mpira, vijana watengenezwe ili wawe na msingi bora toka utotoni!!
 
Jifunze kunyamaza'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…