Live: Kutangazwa kwa mchezaji bora wa soka Afrika

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Leo,katika jiji la Abuja nchini Nigeria atatangazwa mchezaji bora wa soka wa Afrika. Atatangazwa mchezaji bora kwa wachezaji wa nje ya Afrika na yule anayechezea ligi za ndani za Afrika

Katika wachezaji wa nje ya Afrika,wamo akina Mane,Mahrez na Aubemayang Kwa wachezaji wa nje,kati yao yuko Mganda Dennis Onyango wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini

Muda huu,Rais wa CAF Issa Hayatou anahutubia.

Rais wa CAF amemaliza hotuba yake. Kuna burudani inaendelea toka kwa Rising Stars.

========
  • NIGERIA: Mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria na klabu ya Leicester City, Riyad Mahrez ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika(2016) katika tuzo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo katika Jiji la Abuja.

    Washindi wengine wa tuzo katika vipengele mbalimbali ni pamoja na Dennis Onyango(Mchezaji bora wa ndani), Uganda(Timu bora ya mwaka), Nigeria(Timu bora wanawake), Mamelodi Sundown (Klabu bora), Kelechi Ihenacho(Mchezaji bora chipukizi Mwenye kipaji), Alex Iwobi(Mchezaji bora chini ya miaka 23), Pitso Masimane(Kocha Bora), Bakary Papa Gassama(Muamuzi bora), Asisat Oshoala(Mchezaji bora kwa Wanawake)

    Aidha katika utolewaji wa tuzo hizo msanii wa kimataifa kutoka Tanzania,Diamond Platinumz alipata nafasi ya kutumbuiza wimbo wake wa Salome.
https://www.instagram.com/p/BO6WZVmlyIN/?taken-by=jamiiforums&hl=en#
 
Timu bora ya taifa ya Wanawake ya mwaka 2016 ni timu ya Taifa ya Wanawake ya Nigeria aka Super Falcons
 
Klabu bora ya soka Afrika ya mwaka 2016 ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini
 
Mchezaji bora chipukizi na mwenye kipaji Afrika wa mwaka 2016 ni Kelechi Ihenacho wa Nigeria na timu ya Man City
 
Kocha bora wa mwaka 2016 Afrika ni Pitso Mosimane wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini
 
Diamond na Rayvanny wanatumbuiza wimbo Salome muda huu. Ni performance dhaifu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…