Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Shihan Koichiro Okuma (kulia) akijiandaa tayari kuanza semina. Kushoto ni mwalimu wa siku nyingi wa karate Tanzania, Willy Ringo Rwezahura Sensei.
Kama mwenyeji, nami nilikwenda kumpokea Shihan Okuma jana.
Semina kubwa ya mchezo wa Shotokan Karate, ambayo imeandaliwa na chama cha Japan Karate Association/World Federation-Tanzania (JKA/WF-Tanzania), imeanza sasa hivi katika ukumbi wa Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam.
Semina hii ni ya wiki nzima ambayo inawakutanisha makarateka kutoka kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini ukiwa ni mwaka wake wa nane sasa ambapo mkufunzi mkuu wa semina hii ni Shihan Koichiro Okuma (6th Dan) kutoka makao makuu ya JKA/WF Japan ambaye aliwasili jana mchana.
Tutaendelea kuwaletea yanayojiri kila wakati kutoka Don Bosco.
===
Meza Kuu,
Shihan Okuma akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi. Miye wa pili kulia. Mgongo unanisumbua hivyo nimeshindwa kushiriki kwa vitendo, si unajua Karate haina siasa?
Mwalimu mkongwe kabisa wa karate nchini Tanzania, Shihan Dudley Mawala Sensei (7th Dan TKF) naye yupo na hapa anatoa neno la utangulizi.
Vijana wameanza kupasha.
Mambo yameiva, hii ni Heian Shodan Kata, wote wanafanya.
Attachments
-
Gasshuku 16.jpg20.3 KB · Views: 61 -
Gasshuku 17.jpg21.6 KB · Views: 60 -
Gasshuku another group.jpg23 KB · Views: 57 -
Gasshuku demo.jpg105.9 KB · Views: 70 -
Gasshuku demon.jpg17.5 KB · Views: 50 -
Gasshuku demons.jpg20.7 KB · Views: 58 -
Gasshuku Kenyan Team.jpg21.1 KB · Views: 71 -
Gasshuku kumite.jpg25.4 KB · Views: 72 -
Gasshuku Tanzania Team.jpg27.8 KB · Views: 63 -
Gasshuku Uganda Team.jpg20.8 KB · Views: 84