LIVE : maoni ya JF kuhusu katiba mpya

collezione

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Posts
352
Reaction score
178
jamani kutoka na kuwa muda wa kukusanywa maoni ni mdogo, na waTZ wengine wako nje ya nchi, nimeweka thread hii itumike kutoa maoni huru ya katiba mpya.
nawakaribisha kwa michango yenu
 
moja ya vitu ambavyo nataka viwe katika katiba mpya
napendekeza SPIKA wa bunge anapochaguliwa aridhie na awe tayari kujitoa uanachama katika chama chake..tuige mfano wa mabunge ya uingereza na marekani, hii itasaidia demokrasia kukua, na kupunguza nguvu ya upande mmoja bungeni.
 
yah, this is what we need in Tanzania,..we need a neutral SPIKA. miswaada inapita bungeni kwa makosa, uchakachuaji wa wa kanuni za bunge, hoja za ufisadi kuwekwa pembeni..hii inatokana majority na ubabe wa chama kimoja
tuige mabunge ya nchi zilizoendelea, ili kuondoa upendeleo wa upande wowote bungeni
 
Viti maalum vya ubunge vinavyotolewa na rais viondolewe kabisa
 
Chama cha siasa kitakachohubiri na kuchochea fujo na vurugu kwa lengo la kufanya Tz isitawalike kifutwe mara moja.
 
Mimi kwa maoni yangu sioni kwanini kitu muhimu kama hiki cha kutunga Katiba yetu kimepewa muda mdogo sana. Sijui hii haraka ya kutunga katiba katika muda mfupi kiasi hiki inatoka wapi na kwa sababu zipi? Kwa mambo ambayo nimeshayasikia au kuyasoma hadi sasa katika huu mjadala wa kutunga katiba mpya naamini kabisa kwamba Chama Cha Mafisadi/Majambazi wameshauteka nyara mjadala huu na kuhakikisha katiba itakayopatikana itakuwa ni ile ya kuwalinda mafisadi waendelee kututawala milele. Sina imani kabisa na zoezi hili la kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu katiba mpya maana haliko huru kabisa na hivyo Katiba itakayopatikana haitatokana na mawazo mazuri ya Watanzania ya nini tunachokitaka ndani ya katiba yetu. Hii katiba itakayopatikana ni bora tu tuiite KATIBA YA MAFISADI.
 
Chama cha siasa kitakachohubiri na kuchochea fujo na vurugu kwa lengo la kufanya Tz isitawalike kifutwe mara moja.

Yeah......Na chama cha siasa kinachofuga majambazi na kuwafunika huku wakijua ni majambazi kisa kinawafadhili kuendeleza udhalimuna ukibaka wake kifutwe mara moja
 
Mgombea Urais lazime athibitike kuwa ni muadilifu kuanzia kwenye ndoa yake, familia yake hadi kazini kwake.

Mtu asiyeweza kuongoza familia yake hawezi kuongoza taifa.
 
Wagombea ubunge wasiwe na rekodi zozote za kihalifu.
Asiwe mtu aliyewahi kuhukumiwa kwa kosa lolote la jinai.
 
kwenye hili Jk haponi. Hzo nymba ndgo mikoa yte Tz??? Ndo mana unaona nchi imemshnda!
Mgombea Urais lazime athibitike kuwa ni muadilifu kuanzia kwenye ndoa yake, familia yake hadi kazini kwake.

Mtu asiyeweza kuongoza familia yake hawezi kuongoza taifa.
 
Viongozi wote kuanzia madiwani, wabunge, Rais, CEOs, wakuu wa majeshi wawe na nywele za kipilipili yaani Watanzania halisi ambao hawana mchanganyiko wowote wala asili ya wageni.
 
kuwe na mtihani maalumu wa kuchaguwa viongozi ngazi ya wilaya "kama ile ya form 4 & 6" .. kuliko kuteuliwa na raisi, hii itasaidia nchi kuongozwa na watu wenye uelewa
 
Kigezo cha kupiga kura kisiwe umri na akili timamu, upimwe pia uelewa ktk suala zima la uchaguzi, na umuhmu wa kuwa na kiongozi bora
 
Kile kipengele kila mwananchi ana haki ya kupiga na kupigiwa kura.

Msisitizo kwenye kuwepo na mgombea binafsi kiti cha Urais
 
Mimi bado nalia na hiyo tume maalum ya katiba kwanini isitokane na bunge? Naomba kamati hiyo itokane na bunge ndipo angalau inaweza kuwa huru kidogo.
 
jamani kutoka na kuwa muda wa kukusanywa maoni ni mdogo, na waTZ wengine wako nje ya nchi, nimeweka thread hii itumike kutoa maoni huru ya katiba mpya.
nawakaribisha kwa michango yenu
Maoni tutakayotoa yatawekwa wapi????????
Au yataishia humu humu JF, ebu tupe ufafanuzi!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…