Mkuu
the choosen,
Awali ya yote nikupe pongezi kwa kutumia muda wako na raslimali kuja kutoa mwanga kwa vijana kuhusu chuo chao UDSM.
Kama kweli vijana watatumia fursa hii na kuuliza mambo mbalimbali, ni ukweli usio pingika kuwa vijana watakuwa na taarifa nyingi na za muhimu kuhusu chuo chao.
Nitoe wito kwa vijana wote wa mwaka wa kwanza watarajiwa; ni vyema mkaichangamkia hii fursa kwa kuuliza maswali, chuo kikuu kuna changamoto nyingi sana, hivyo ni wakati wenu huu kuuliza ili mtambue ni namna gani mtambana na changamoto za chuo na kufanikiwa kuhitimu ili muweze kufanikisha ndoto na malengo yenu.
Ni hayo tu vijana.