Wakuu.
Leo kuna mchezo wa kirafiki kati ya Coast union ya Tanga na Simba ya DSM, mpaka
sasa si coast wala simba
ambaye ameliona lango la
mwenzake. Mpira ni pamumziko sasa hivi.
Coast union wameonyesha kiwango kikubwa
cha mpira wakiwatumia wachezaji wao wakongwe Haruna Moshi Bobani, Juma Nyoso, Uhuru Selemani, Shabani Kado na Jerry Santo.
Upande wa Simba mpaka sasa
mchezaji aliyeonyesha kiwango cha juu ni
aliye kuwa mchezaji wa zamani wa Azam ambaye alifanya majaribio na kufuzu timu ya Jomo Cosmoss ya Afrika kusini, Abdulhalim Hamoud.
Nitazidi kuwajuza.