Na Zainab Nyamka, Dar
Timu ya Kauzu Fc imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali michuano ya Ndondo Cup, baada ya kuifunga Kibada Fc bao 1-0 katika mchezo wa robo Fainali iliopigwa jana jioni kwenye Uwanja wa Bandari, jijini Dar es Salaam.
Bao hilo pekee lilifungwa na Rashidi Roshwa, katika dakika za lala salama.
Akizungumza na mtandao huu baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa
Kauzu Fc Mashaka Said, alisema kuwa wamefurahia matokeo hayo na kutinga
Nusu fainali mwaka huu ba kusema kuwa wanajipanga na maandalizi ya
kutosha ili waweze kuchukua hasa baada ya mwaka jana kufungwa na
waliokuwa mabingwa Faru Jeuri.