LIVE Updates: Rumble in Dar Season 2

LIVE Updates: Rumble in Dar Season 2

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
18,585
Reaction score
16,780
Wakuu, Tuko Next Door Arena.
Kuna mapambano ya Ndondi yanaendelea hapa.
Mpaka Sasa mapambano ya Raundi nne yameisha Mawili na Yote Tz tumepoteza.

Lets Go. Pambano la Tatu sasa.
Naona Mkongo anakipiga na Mtz hapa... Twende sawa.

Hamis Palasunga anakipiga sasa.

====
RUMBLE IN DAR: MWAKINYO NA IBRA CLASS WAING’ARISHA TANZANIA

Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo ameshinda kwa KO dhidi ya Bondia Antonio Mayala wa Angola. Pia Ibrahim Class ameibuka mshindi dhidi ya Sibusiso Zigange wa Afrika Kusini

Mabondia wengine wa Tanzania walipigana katika ulingo wa Next Door Arena walipoteza mapambano yao, akiwemo Shaabani Jongo aliypigwa KO na bondia wa Nigeria Olanrewaju Durodora

Mtanzania Imani Daudi Kaway amepikwa kwa KO na Bondia Chris Thompson kutoka Afrika Kusini, pambano la uzito wa Juu (Heavy weight). Ardi Ndembo wa DR-Congo ameshinda kwa KO dhidi ya mtanzania Hamisi Palasungulu

Mtanzania Leila Yazidu amepoteza pambano lake dhidi ya Joana Nwemerue kutoka Bulgaria. Pia Daniel Matefu amepoteza pambano lake dhidi ya Mbulgaria Pencho Tsvetkov
 
Andre Ndembo from Congo brazavile anafanya maajabu hapa.

Hamisi anapigwa sana.
Sijui kama ataweza kuendelea
 
Inatokea knockout ndani ya sekunde ya 45 ya mchezo.
Hamisi Palasunguru Kapigwa katika round ya Kwanza kwa Knockout matata sana.
 
Shindano la 4.
Chris Thomson Vs Iman Kaway.
Tuone tena inakuaje hapa ndani ya next Level arena.
 
Mpaka sasa sisi watanzania tumepoteza Mapambano 3
 
Round ya Kwanza ndio inaanza hapa.

Pambano hili lina round 6.
 
Round ya 1 inaendelea.
Iman anajitahidi hapa, Msouth ni mrefu kidogo hii inamsaidia sana.

Iman anarusha makonde hayamfikii vizurivChris
 
End of Round 1.
Iman amejitahidi makonde kama mawili lakini dhaifu yalimfikia Chriss
 
Iman kama vile anazidiwa hapa kwa kweli.
Kesharuhusu makonde kadhaa hapa
 
Kwenye hii Round ya 3 Iman anajitahidi sana ila anazipokea pokea.
Sijui inakuwaje hapa.
 
Round ya 3 inakuwa ngumu tena kwa Iman Kaway. Anajitahidi lakini naona kama msauzi anajitahidi zaidi.

Iman kpigwa chini hapa.
Kanyanyuka, mwisho wa Round ya 3.

Inatia wasiwasi kidogo hapa.
Msauzi kampushi mtz
 
Back
Top Bottom