OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
AJENDA ZA MKUTANO MKUU MAALUMU WA MABADILIKO YA UENDESHAJI WA KLABU YA SIMBA
Kuhakiki idadi ya wanachama waliohudhuria mkutano
Kufungua mkutano
Kuthibitisha ajenda
Hotuba ya rais
Kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Simba
Kujadili mapendekezo ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Simba
Kupiga kura ya mapendekezo ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Simba .
Majumuisho ya Ajenda no 7
Kufunga mkutano
Update 1
Rais Simba awaomba wanachama kupitisha mfumo wa mabadiliko
Kaimu rais wa Simba, Salim Abdallah amewaomba wanachama wa Simba kupitisha mabadiliko ya uendashaji wa klabu yao.
Salim ameyasema hayo katika hotuba yake ikiwa ni muda mfupi kabla ya wanachama kupigia kura mabadiliko hayo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.
Wanachama zaidi ya 1,000 wamehudhuria mkutano huo ambapo Kaimu Rais wa Simba amesema endapo watapitisha mabadiliko hayo itatangazwa tenda.
Update 2
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Hamis Kigwangala amesema mabadiliko yanayokwenda kufanywa na Simba yana faida.
Dk Kigwangala ambaye ndiye mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa Mabadiliko ya Uendeshaji ya Klabu ya Simba amesema mabadiliko ambayo klabu hiyo inakwenda kuyafanya yanafaida.
"Klabu nyingi za soka duniani zinaendeshwa kibiashara, sisi tulichelewa na bila shaka Simba itafungua njia na wengine watafuatia hapa nchini," alisema Dk Kigwangala.
Update 3
Lengo la klabu ya Simba ni kuwa na shule ya michezo (Academy) viwanja vya michezo na usajili mkubwa"- kaimu Rais wa Simba Salum Abdallah Akihutubia katika mkutano unaondelea sasa hivi
Update 4
"Kukaribisha wawekezeji si kuuza timu, kuna utaratibu unawekwa wa uwekezaji lakini sio kuuza timu kama ambavyo wengi wanadhani
Klabu ya simba itakuawa na uwezo kuboresha muundo wa kiutawala na kujiwezesha kitaalmu, itaweza, kulipa mishahara, kutengeneza Academy na miundombinu mingi inayo hitajika katika klabu kubwa kama Simba"- katibu wa kamati ya mabadiliko bwana Selemani
Update 5
Wanachama wapitisha mabadiliko Simba
Wanachama wa Simba wamepitisha mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo kwenye mkutano mkuu maalumu uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Jumapili.
Wanachama hao wamebariki mabadiliko hayo baada ya kupiga kura za kukubali au kukataa ambapo ni mwanachama mmoja kati ya ya 1,217 alipinga.
Katika mkutano huo uliofanyija jijini Dar es Salaam leo Jumapili, wanachama hao walipiga kura ya wazi wakihojiwa na Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah