Utitiri wa mashabiki wa Yanga jana
Ijumaa ulijazana kwenye Uwanja wa
Bora, Kijitonyama, Dar es Salaam
kumwangalia mshambuliaji wao
mpya, Okwi ambaye alianza mazoezi
na kikosi hicho ambapo kocha mkuu
wa timu hiyo, Mholanzi Ernest
Brandts amekiri kwamba atamtumia
mchezaji huyo kwenye fowadi.
Brandts alifafanua sababu ya
kumchezesha kama straika na winga
kwa sababu ana sifa zote, ni
mwepesi ana kasi, anajua
kutengeneza nafasi za mabao na
anafunga pia.
Alisema: Uwepo wa Okwi kikosini
mwetu ni faraja. Okwi ni mchezaji
mzuri na ninafuraha kuwa naye
kikosini kwa sababu ana kila sifa za
uchezaji. Okwi ni mwepesi ana kasi
katika uchezaji, anajua kutafuta na
kutengeneza nafasi za kufunga lakini
pia yeye ni mfungaji mzuri wa
mabao, ndiyo maana tukamtafuta na
kumleta Yanga.
Alipofika tu, mashabiki ambao
walikuwa wamewahi na kufurika
maeneo hayo, walikuwa wanaimba
nyimbo za shangwe wakimpokea,
Okwi, Okwi..
Na kabla ya kuanza mazoezi, Brandts
alimtambulisha, Okwi kwa wachezaji
wenzake na benchi la ufundi:
Tumepata ugeni wa mwenzetu
hapa, nafikiri wote mnamjua, Okwi
tutakuwa naye kwenye timu,
mumpe ushirikiano.
Wakiwa katika mazoezi, mchezaji
ambaye alikuwa karibu sana na Okwi
ni Said Bahanuzi ambaye walikuwa
wakizungumza na kucheza ingawa
baadaye alizungumza na kucheka na
wengine.
KOCHA SIMBA
Kochawa Simba, Zdravko Logarusic
amesema amekaa na wachezaji
wake na kuwaweka sawa kisaikolojia
huku akidai mechi za wapinzani wa
jadi huwa hazimsumbui hata kidogo
na anaamini asilimia 90 kikosi chake
kitaibuka na ushindi.
Simba na Yanga zinapambana katika
mchezo utakaoanza saa kumi kamili
jioni.
Maandalizi yetu ni mazuri wachezaji
wote wako vizuri tayari kwa mchezo
huo ambao utakuwa mgumu, mzuri
na wenye ushindani sana. Nimekaa
na wachezaji wangu na nimewaweka
sawa na kuwambia kuwa hawatakiwi
kuhofia hiyo mechi, tutaingia
uwanjani kwa kasi kuanzia mwanzo
hadi mwisho wa mchezo ili
kuhakikisha tunashinda hiyo mechi,
mimi sina presha nayo kwa sababu
nazijua mechi za wapinzani hivyo
hazinisumbui, alisema Loga.
Aliongeza: Kutokana na ubora wa
timu yangu na aina ya wachezaji
nilionao hiyo mechi tunashinda,
amini usiamini, hatuogopi yeyote,
tunakwenda uwanjani kuonyesha
soka la kiwango, mashabiki waje kwa
wingi kutusapoti kwani wao ni
mchezaji wa ziada uwanjani.
Mechi ya mwisho timu hizo kukutana
ilikuwa Oktoba 20 mwaka huu na
kutoka sare ya mabao 3-3, Yanga
walikuwa wa kwanza kufunga mabao
yao lakini Simba wakaibuka kipindi
cha pili na kusawazisha yote