Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Kama we umesema ngoja na Mimi nijitahidi japo kuna muda hua natamani kupiga TV teke [emoji28]
Dogo anakera mno aisee mpaka basi.

Klopp hua ana jicho la kuona raw talent hakuna mchezaji under 30 aliesajiliwa Liverpool akiwa staa.. Ni Thiago tu alisajiliwa akiwa ready made wengine wote Klopp amewajenga mwenyewe tazama wengi walisema Mane tulichekwa, VVD tulipigwa, Salah one season wonder, Allison overrated, Gini, Robbo nk nk wote hao tulichekwa mno lakin muda tu wakawa world beaters hakuna alitamani kukutana na Liverpool kwa kutazma hao wachezaji alivyowaleta Klopp nakua na imani hakubahatisha kwa Nunez kutoa ela zote zile... Nina imani na Klopp.

YNWA
 
hivi u21 yetu haina namba 3 akaaminiwa akapewa nafasi

Tuna Calum Scanlon

Amecheza Carabao mechi moja hivi na Europa alipata some minutes. He is good ila kuaminiwa moja kwa moja ngumu.

Gomez will be our LB, Robbo anarudi January. Good thing Gomez is in a good shape by now ( i fear less).

But these injuries zimetuandamana sana. Rotation muhimu sana, we need

Macca
Jota
Thiago
Bajcetic
Robbo

Asap, ili kuwapumzisha wengine. And the rest kuwa fit we can still Challange.

But i real don know enough kama tutaingia sokoni january hii, na kama tutaingia basi ni mmoja au wawili. Klopp ameshaanza “the right time, the right player”.
 
Duh... Basi dunia haiko fair mi nikimuonaga Tu Nunez nahisi Dalili za kupoteza game

Vile mnamsema Nunez as if ni Defender au Gk. Give him a break.

Salah tuliona miss vs Westham (you cant judge him alot, among all time top scorer pale EPL).

See vs Arsenal that missed from TAA (its not a debatable) ingekuwa Nunez angekaangwa balaa.

Ila Nunez anakosa magoli mepesi ila uwepo wake unamchango mkubwa kuliko wa Diaz and Gakpo Currently.
 

He will Click. At LW namuona anatupa vitu muhimu pia. Its time Klopp amjaribu Gakpo as CS With less false nine role.
 
Kabisa… Napenda vile yupo positive, Halafu huwa anawapopoa wapinzani kwa hiyo kwa upande huo tumepata M/Kiti.

Kudos kwake.

Merry Christmas
🤣 🤣 🤣 She is the one haha...utadhani wapo Saint Anne 10 kumbe mmoja tu 🤣.

YNWA
 
So change in MF has changed our new season ama namna gani..
My views..
VVD is back na awamu hii aidha by luck or huko mazoezini ama vyote amekua na combination bora na mabeki wenzake akiwemo dogo Quansah, hii imetupa solid foundation kujenga ukuta imara regardless anacheza nani.
MF imekua a bit progressive na kua hatuna choosen heir wa Fabinho wamekua wakisaidiana mno namna ya kusonga mbele pamoja na kuzuia pamoja. Domy S amekua na msimu wa kwanza safi kabisa in fact amezidi our expectations.. Pia hawa ma dogo kukumbali kwa moyo mmoja kucheza nafasi ama mfumo tofauti na walipotoka imetupa balance kiasi chake... Wachezaji kukumbali na kujituma uwanjani kama Macca playing DM ambayo alipotoka alikua Caicedo lakini hapa Liverpool he is there executing gaffers plan by th action ni jambo njema sana....
Forward line wamekua positive kwamba sio kufunga tu kuna count mbali pia kutengeneza kwa ajili ya wengine.. Hii imetupa new hope na kuwapa mtihani wapinzani wasijue nani wamkabe nani wamuache... Utaona Jones, Elliot, Domy, Trent hao wanafunga hii inapunguza presha kwa ma forwards...
Kuwaachia Henderson, Keita, Ox ilikua maamuzi sahihi.. Tuna MF changa ina miguu fresh kabisa kwa ajili ya mapambano.
Benchi nalo kwa sasa limesheheni vipaji... Tazama Jota na Diaz nk wapo benchi hii inatupa fursa kubwa wanaonza wakichemka basi Klopp chap anafanya sub zamani haya tuliyaona kule kwa Kipara lakin sasa tuna utajiri wa benchi...
Klopp kukumbali kuwapa academy kids some minute kama Quansah, Doak na hii imetusaidia sana ku manage hawa wachezaji wenye historia ya kuumia kama Konate ambaye kukaa fit ni ishu lakin akiwa well managed ku rotate na Quansah naamin atakaa sawa.
Kuongezeka kwa ushindani wa EPL nako kumeleta msukumo mpya kwamba hakuna favourite wa top 4 kila mmoja ashinde mechi zake, tazama Aston Villa walivyombana Manchester City yaan kwa mara ya kwanza kikosi cha Kipara walipiga shot on target 2 au 3 mechi yote hii inaonyesha namna gani walimu wameamka na kutoa mbinu sahihi kwa wachezaji wao...

Wengi walikua na wasiwasi na msimu huu tutakua pambaya...

Nina imani na vijana.

YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…