Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Najua mashabiki wa Chelsea watakuwa wamefurahishwa na performance yao ila ubao unawaumiza.

Kwenye mpira strength yako inaweza kuwa weakness yako at the same time.

Walijua build up ya LFC msingi ni Double pivot Gravern & Jones, plus CB’s akaja na mbinu ya narrow high pressing, wanatengeneza umbo la square yaani Gravern na Jones wanazungukwa na watu wanne, halafu nyuma yao wanasima wachezaji wawili au mmoja ili kuzuia spaces za MF’s na Attacks (LW, RW, AMF) wasipokee mipira. Wali win sana kwa sababu walikuwa na two defensive minded MF’s Lavia na Caicedo (binafsi kati ya Caicedo na Lavia all the way namchukua Lavia), jamaa kazuri sana with the ball.

Anyway, kwenye mbinu yao hiyo, wakawa wanatengeneza gap kati ya MF na defenders, sasa hapa LFC wakaamua kutumia “weakness within the strength” yes mmetuzuia kuanzia juu lakini huku chumbani kwenu pako wazi we will try na hili. Hivyo Slot akaamua Jota ndiye awe ufunguo wake (mzuri kupokea mpira akilipa goli la mpinzani mgongo), win your duels sambaza mipira kwa LW/RW/AMF (mbinu za kina Tony pulis enzi hizo, kina Moyes na Everton yake ile, kina Big Sam). Somehow Jota tried alot ndio maana injury aliyoipata ilikuwa long ball kuwaniana na Tosin aka mbeat akatangulia ikatangulizwa BOOM foul & yellow kwa Tosin.

Alipotoka Jota baada ya injury, tuka switch kwake tumtumie Salah, again it worked very well, tukapata goli la pili kwa mbinu hiyo. “Within your strength there is a weakness and i will use it”.

2nd goal a world class GK angeucheza ule mpira vizuri tu, kwanza it was poor touch kwa Jones lakn Sanchez didn’t react at a right time, Jones akatumia udhaifu huko and beat Sanchez. 2-1.

An offside goal, it couldn’t be, only if Jones had released that ball immediately. VAR Penalty cancelation yes it was correct decision, not because we won but Sanchez aliugusa ule mpira before kumgusa Jones, but Jones should have scored that goal. Szobo the same as Jones akili na miguu vinapishana kimaamuzi.

Shabiki anakuambia wasingemshika Palmer wangeona, ? Hahah thats football lazima ujue uimara wa mpinzani ni wapi na udhaifu ni wapi ili mminyane hapo hapo, Kudos to Jones alitembea na Palmer muda wote, kudos to Maresca alistick na plan yake ya high pressing narrowly with loads of players.

Again:- Jones and Gravern as Ball carries kwenye miguu yao ndio ilikuwa Silaha nyingine kwa Slot, im pretty Sure kama angecheza Endo angeweza ku struggle kwa structure ya Slot ya jana na strategy ya Maresca jana. Ilikuwa ni mechi ambayo unahitaji watu wanyumbulifu sana wenye uwezo wa kucheza na tight spaces. Wazuri miguuni wakiwa na mpira, hawaogopi kuchukua mpira popote, Jones & Gravern walitu offer hivyo vitu jana. Thats why unaona Slot anadunda even without Natural DM.

Its a pleasure to a new manager kushinda 10/11 games ndani ya msimu wake wa kwanza. Lets keep hope for the best.

My concern je, Slot atajipanga vipi na pressure ya kuwa kileleni? Japo hajawahi kuonja joto hilo we shall see, maana last season joto lilituzudi tukashindwa kuhimili pressure.
Ubingwa una mambo mengi sana ndani yake. Jana nilimuona akiwa furious kwenye tukio la foul dk za 20 hivi, ilikuwa ni Salah ile kama sijakosea, after the match niliona akiwafuata marefa witg full face of furious, bahati wakamzuia bana wewe njoo huku, umeshashinda mengine achana nayo.


Mechi ngumu ya kwanza imemalizika with 3 points in the bag.

Next CL Match, then twende pale Emirates tukavaane na Artata vilivyo.

Up Liverpool
Go reds
Ynwa’
 
Hata nyie mna kocha mzuri mngewapa muda Palmer na Madueke tungeongea mengine but kocha wenu akaja na plan ya kublock Palmer na kuweka watu wengi upande wa Madueke
Kwa kweli tuna utulivu sana chini ya Slot especially wakati tunashambuliwa vijana wanaelewa vyema wapi wasimame... Tazama Jones alikua analinda njia za Palmer na muda huo huo tukishambulia yupoo.

YNWA
 
[emoji599] 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: Virgil van Dijk confirms talks ongoing with Liverpool over his contract! [emoji837][emoji2399]

“Yes, talks are ongoing with the right people to discuss my new contract at Liverpool”, Virgil has told the media.

“When it’s time to make a decision, you will know it all”.

“But now my full commitment and full focus is only on Liverpool, to be successful this season all together”.
 
Mashabiki wa Liverpool mnajua kuuchambua mpira vizuri kwenye hii angle mpo vizuri sana
 
Kwa kweli tuna utulivu sana chini ya Slot especially wakati tunashambuliwa vijana wanaelewa vyema wapi wasimame... Tazama Jones alikua analinda njia za Palmer na muda huo huo tukishambulia yupoo.

YNWA
Ukiangalia lineup yenu wala haitishi wachache tu ndio wenye majina na hata wachezaji mnaowasajili hawana hata majina ila mkiwa uwanjani vitu viwili tofauti mna kuwa wafanisi haswa na unasema hapa kuna team ndio maana ya kuwa na kocha mzuri na proper management.
 
Mnataka majina gani 😂😂😂
 
Kelleher ni golikipa wa dunia nzima
 
Hata nyie mna kocha mzuri mngewapa muda Palmer na Madueke tungeongea mengine but kocha wenu akaja na plan ya kublock Palmer na kuweka watu wengi upande wa Madueke
Yule jamaa wenu wa the blues mwenye id ya namba mapank Yuko wapi?
Alijaaga humu sana akitusumbua
 
Hapo kwa palmer nimekuelewa sana. Ukitazama mechi za chelsea vs briton na wolves kuhusu huyu palmer ulichokisema kina make sense.
 
Nu lineup yenu wala wachache tu ndio wenye majina na hata wachezaji t hawana hata majina ila mkiwa uwanjani vitu viwili tofauti mna kuwa wafanisi haswa na unasema kuna team ndio maana ya kuwa na kocha mzuri na proper management.
Slot kaangalia sana clip za Liverpool last season na akaja na mbinu zake kwamba gegenpresin ya Klopp ina changamoto zake ukiwa huna ballers wakat unacheza vs ballers kama Chelsea hivyo mbinu ni kupiga counter attack na hakika tumefanikiwa...

YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…