LIVERPOOL HUU NI WAKATI WENU KUNYAKUA KOMBE

Efendi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
314
Reaction score
438
Mara ya mwisho Liverpool kuchukua ubingwa wa Uingereza ilikuwa siku ya Jumamosi, Aprili 28, 1990 baada ya kuifunga QPR goli 2-1.


ANC ilikuwa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini.

NCCR Mageuzi lilikuwa vuguvugu la kutaka mabadiliko ya katiba Tanzania.

Rais wa Marekani alikuwa George Bush mkubwa.

Soda moja ilikuwa shilingi 40/=

Tanzania Bara ilikuwa na mikoa 20.

Stendi ya mabasi ya Mikoani ilikuwa Kisutu na Mnazi Mmoja.

Palipo na Ubalozi wa Marekani palikuwa Drive Inn Cinema.

Kasper Schmeichel hakuwa amezaliwa lakini mwaka jana kachukua ubingwa na Leicester City.

Jose Mourinho hakuwa ameanza kuwa kocha lakini katwaa ubingwa huo mara 3.

De Gea hakuwa amezaliwa lakini katwaa ubingwa huo.

Noti ya juu kabisa Tanzania ilikuwa shilingi 1000/= na shilingi 10/= ilikuwa ya noti.

Rais mstaafu Benjamin Mkapa alikuwa waziri, JK alikuwa naibu waziri na JPM alikuwa mwalimu wa sekondari. Wote hao wameshakuwa marais.

Kumbi maarufu za burudani Dar zilikuwa La Prima, Bahama Mama na Mbowe. Na moja ya bendi maarufu ilikuwa Bima Lee Orchestra.

Msemo maarufu ulikuwa 'la kupalama la kuchumpa' na msichana aliitwa 'kishtobe'.

Sanduku la Posta ndo ilikuwa kitu cha kurahisisha mawasiliano na duniani tulikuwa na penpal friends.

Sir Alex Ferguson alikuwa na miaka 3 tu toka awe kocha wa Man United. Ameshastaafu baada ya miaka 27 na sasa ni miaka minne tangu astaafu.

Man United ilikuwa imeshatwaa ubingwa wa ligi mara 7 tu na Liverpool mara 18. Lakini leo hii Man United keshatwaa mara 20 na Liverpool bado hizo hizo 18.

Sehemu kubwa ya Ubungo ilikuwa pori na Sinza bado kulikuwa na mashamba ya mpunga.

Viwanda maarufu vya nguo vilikuwa Sunguratex na Urafiki. KTM Mbagala haikuwepo. Kwanza Mbagala yenyewe ilikuwa porini kabisa.

Timu maarufu kwenye ligi ya Tanzania ukiachia Simba na Yanga, zilikuwa Pilsner, Sigara, Tukuyu Stars, Lipuli, Ushirika Moshi, Pamba, Nyota Nyekundu, Milambo, Reli, MECCO, Coastal Union, Pan African, Ujenzi Rukwa na RTC Kagera.

Marijani Rajab alikuwa bado hai.

Diamond Platinumz hakuwa ameanza hata shule ya vidudu.

Kiongozi aliyekuwa akiogopwa duniani alikuwa Saddam Hussein.

Stori maarufu Tanzania zilikuwa za Willy Gamba. Jarida maarufu zaidi lilikuwa Sani la kina Bawji na Nico ye Mbhago na Tanzania Film la Faraji H H Katalambula.

Mchoraji maarufu zaidi alikuwa John Mathias Kaduma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Liverpool wanatatizo la nguvu za kufika kileleni,na saiz watazidi kurudi nyuma tu
 
Umesahau kutuambia mitandao maarufu kipindi hicho
 
Liverpool Ameanza mwaka vibaya atatobolewa sana tu
 
Umesahau haya

CCM ndio kilikuwa chama pekee cha siasa (Monoparty) hapa Bongo

Moja ya masharti ya kujiunga chuo kikuu ilikuwa lazima uwe na kadi hai ya CCM

Mengine ongezeeni wenyewe____________________________________
 
Endeleeni kuishi kwa historia hivi hivi, ila tukikutana nanyi tunawapiga kuanzia 5, 3 na mwezi May tunabeba vikombe vyote Uefa, Epl, FA.
Ahahaaaah...
Itakua vizuri...
Ila ni vyema ukakesha ukiomba...
Pia usisahau kufunga..!
 
Endeleeni kuishi kwa historia hivi hivi, ila tukikutana nanyi tunawapiga kuanzia 5, 3 na mwezi May tunabeba vikombe vyote Uefa, Epl, FA.
Ahahaaah...
Ulikua unamaanisha nini hapa Kiongozi..!?
Mjifunze kuwe prudent katika uchambuzi wa mpira,weka hisia zako pembeni fanya uchambuzi..!
Kwa huu uchambuzi wenu wa kutumia hisia,ikifika May tutakua na makaburi mengi sana ya kufukua..!
 
Mods unganisheni na Uzi maalum wa LFC

Naona mgeni anaanzisha tu uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…