Liverpool kuchukua ubingwa EPL, pongezi zangu nazielekeza kwa Kloop

Prof young bernie

New Member
Joined
May 4, 2020
Posts
1
Reaction score
1
Wanajamvi, msimu huu team ya Liverpool imechukua ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza baada ya miaka 30 na ni mara ya kwanza tangia ligi hiyo ianzishe kwa namna tofauti kidogo na ilivyokuwa mwanzo.

Nimejaribu kutafakari ni yupi anastahili sifa katika hili nimeona si mwingine ni mwanaume wa Kijerumani Jurgen Kloop ambaye ameibadilisha Liverpool kwa kiasi kikubwa mpaka kuwa team tishio barani Ulaya na Duniani kote kiujumla.

Jurgen alivyokuja Liverpool kwanza kabisa hakuwa na hulka ya kusajili wachezaji wakubwa bali aliwatengeneza hao aliowakuta na kuongezea wachezaji wachache tena wa bei za soda huku akijenga ukaribu nao kwa kiasi kikubwa na kumfanya kila mchezaji apaone Liverpool ni sehemu salama kwake kimaisha na kimpira.

Kloop alimaliza mchezo pale alipowasajili wachezaji kama Alison Ecker, Mo Salah, VVD, Gin Wunldun, Fabinho na kuwaamini wachezaji kama wakina Origi, Milner, na Henderson.

Kusema ukweli, Kloop amekuja Liverpool ikiwa ni sehemu sahihi kwake na muda sahihi na kiujumla management ya Liverppol kati ya sajili zote walizozifanya kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita usajili mkubwa na bora ni pale walipoamua kumsajili Kloop awe manager wa club ya Liverpool.

Viva liverpool, viva Kloop, viva Kops wote duniani mmepata mlichostahili.

Viva Benard Kabuhaya shabiki no 1 wa Liverpool Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…