Liverpool na kilele cha mafanikio: Tunajifunza nini?

Liverpool na kilele cha mafanikio: Tunajifunza nini?

EZZ CHEZZ

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
1,230
Reaction score
1,352
Pongezi nyingi kwa wanafamilia wote wa Liverpool ulimwenguni kote. Ni dhahiri kuwa sasa hakuna miongoni mwao anayetembea peke yake. Haikuwa kazi rahisi. Ni mradi wa zaidi ya miaka mitano. Ndiyo, tangu waanze rasmi mchakato wao wa kurejea kileleni, pale walipomsajili mbishi Klopp.

Binafsi nimejifunza yafuatayo:

1. Mafanikio ni mchakato mrefu unaohitaji uvumilivu mkubwa
Hakuna mafanikio ya mara moja. Hakuna pia njia ya mkato. Angalia namna Liverpool walivyotengeneza malengo yao. Angalia pia namna walivyotafuta kocha atakayeendana na malengo yao. Wakaanza kumpa wachezaji aina inayotakiwa na mfumo wao mmoja baada ya mwingine. Tazama uvumilivu wao. Je, ingekuwa Man United, Klopp angekuwepo mpaka leo? Chelsea? Arsenal? Simba? Yanga? Si rahisi. La hasha, angekuwa kesha timuliwa.

2. Suala la usajili: Benchi la ufundi vs matakwa ya klabu
Liverpool wametuonesha kuwa ili klabu ifanikiwe (uwanjani) sharti kuwe na kemia nzuri baina ya klabu na kocha. Kwamba kocha na klabu watakubaliana aina ya mchezaji wanayemtaka kwenye eneo husika na kisha atasajiliwa. Na siyo kocha anataka hiki anapewa kile. Angalia namna ambavyo United kwa mfano. Kocha anaweza mtaka huyu akaambiwa hafai. Mwaka mmoja baadae yuleyule anasajiliwa wakati mambo yashaharibika. Rejea suala la Maguire. Arsenal pia Arteta ashaanza kulalamika kuwa akiagiza kuku anapewa bata.

Hapa kwetu bongo ndiyo shida kabisa. Klabu zetu zote hufanya usajili wa wachezaji bila kujali benchi linataka nini. Angalia Simba walivyosajili mwaka jana. Katika wachezaji wote ni mmoja tu aliyetakiwa na kocha (Kahata). Wengine wote ni utashi wa akina Manara.

Tazama Yanga wanavyohangaika kulazimisha makocha kufanya kazi na wachezaji ambao hawakuwasajili wao. Ni kocha njaa pekee ambaye atafanya kazi kwenye mazingira kama hayo. Kupata mafanikio kwenye mazingira hayo ni miujiza.

3. Usajili na falsafa ya klabu
Kwamba timu sharti isajili wachezaji wale tu wanaoendana na falsafa na itikadi za klabu. Hii ni kuanzia kwenye mtindo wa uchezaji mpaka kwenye hulka za wachezaji. Liverpool kwa mfano, ni timu inayocheza mchezo wa kasi hasa kutokea pembeni. Hivyo kila mchezaji aliyesajiliwa nayo ni yule ambaye ana-fit mfumo huo. Angalia wingers wao mpaka full backs. Hata viungo wakabaji ni wale wenye kasi ya mchezo na wenye pumzi ya kuweza kuhimili dk 90.

Kwa upande wa hulka pia wamesajili wachezaji wazuri lakini wasiojikweza pale wanapokuwa juu. Angalia timu zingine kama United ambazo hapo katikati zimesajili wachezaji wasioendana na falsafa na itikadi zao pamoja na kuwa wana vipaji. Martial, Pogba, Sanchez, nk.

Wewe umejifunza nini?
 
Nimejifunza kuwa kwa miaka mingi Liverpool hawakuwahi kunusa ndoo Leo Chuma JPM kaingia Liverpool kalamba dodo.
 
Back
Top Bottom