Liverpool waipiga Chelsea, wabeba ubingwa wa FA Cup

Liverpool waipiga Chelsea, wabeba ubingwa wa FA Cup

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Liverpool imefanikiwa kushinda Kombe la FA baada ya kuifunga Chelsea kwa penati 6-5 katika fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Wembley, leo Mei 14, 2022.

Hadi dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa 0-0, ilibaki hivyo hata baada ya kuongezwa dakika 30. Mason Mount alikosa penati ya mwisho kwa Chelsea kisha Konstantinos Tsimikas akaifungia Liverpool penati ya ushindi.

Liverpool ambao walitwaa Carabao Cup 2022, watacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid, pia wanayo nafasi ya kutwaa Premier League licha ya kuwa nyuma kwa pointi tatu dhidi ya Manchester City.
 
Back
Top Bottom