Liwale: Watoto wadogo wabambikiziwa kesi ya "unyang'anyi" wa kutumia silaha

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
LIWALE: WATOTO WADOGO WABAMBIKIZIWA KESI YA "UNYANG'ANYI" WA KUTUMIA SILAHA.

Watoto SAID HASSAN BADI, 14 (Kushoto kwangu) na SALAMA HASHIM MBWANA, 14 (Kulia kwangu) - (wote wanafunzi wa kidato cha kwanza) wakiwa mahakama ya wilaya ya LIWALE mara baada ya kusomewa mashtaka kwenye kesi zaidi ya tatu. Katika kesi moja watoto hawa wanatuhumiwa kuvamia duka, kulivunja, kuona na kumtishia mwenye duka (mwanaume) watamuua kwa silaha.

Nilipoongea na watoto hawa nilishangaa sana, huyo wa kiume anasema siku ya matukio ya wananchi kufanya vurugu yeye alikuwa anaangalia mpira, aliposikia milio ya risasi majira ya jioni alikimbia kutoka ukumbini, njiani akakutana na mjomba wake ambaye ni diwani wa CCM, mjomba wake akamuuliza anakimbia nini? Akamjibu kuwa ameambiwa kuwa kuna vurugu hivyo anakimbilia nyumbani. Diwani wa CCM akamwambia anawajua vijana waliomjulisha kuhusu vurugu? Kijana huyu akajibu hawajui, ndipo mjomba mtu(diwani) akaanza kumpiga makofi, na mwisho wa siku kijana huyu akakimbilia kwao.
Keshoye akaamkia shuleni, akiwa shuleni mjomba wake akaja na polisi, wakamkamata. Hajui lolote kuhusu matukio hayo lakini anasomewa shtaka la kuona kwa kutumia silaha usiku wa manane.

Huyu SALMA(msichana), anasema siku moja baada ya matukio ya LIWALE, polisi walifika nyumbani kwao(Yeye Salma na mama yake wanasimamia nyumba ya ndugu yao yenye wapangaji). Polisi walipofika wakamkamata mpangaji mmoja na kusachi chumba cha mpangaji huyo. Baadaye polisi wakaondoka na mpangaji huyo pamoja na DRYER ya Saloon na kiti cha Saloon(vinavyosemekana kuwa vya wizi).

Baada ya muda kidogo, polisi wakarudi na wakaanza kumpiga sana msichana huyu na mama yake, wakawakamata na kuwaweka Rumande. Yule mpangaji alokutwa na vitu vya wizi aliachiwa kesho yake na hajapandishwa kizimbani.

Hadi mtoto huyu na mama yake wanafikishwa mahakamani hawakuwahi kujua kosa lao ni nini.
Wamefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kesi 4 tofauti. Katika kesi mojawapo, mtoto huyu anatuhumiwa kwa kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha na haina dhamana.

Chama kimechukua hatua za dharura za kuweka mawakili ili wananchi wanaobambikiziwa kesi wanusurike. Inasikitisha sana. Polisi watumika vibaya.
 
Mimi na layman,

hivi sheria zinaruhusu watoto wa umri chini ya miaka 18 kushitakiwa?

Je kuna ushahidi wowote walikutwa nao (silaha, picha za video walipokua wanafanya ujambazi)
hivi kweli vjana wadogo hivyo wanaweza kufanya tukio lolote? Kwangu mimi hata kama wa AK47 ntawashinda kwa jinsi walivyo.

Hao watoto wangekuwa ni trained rebel group ningekubali ila ni wanafunzi tena kidato cha kwanza. OMG

serikali iwe makini kwenye hili
 

Hii intelijensia ina walakini kweli kweli.
 
Polisi wa nchi hii huwa nawafananisha na maroboti, hawana hata uwezo wa kufikiri, sijui wakoje!!
 
Wataalamu wa nasaha kuna hali wanaita defence mechanisms, moja ya hizo defence mechanisms ni "DISPLACEMENT". Displacement hutokea pale, bila kujitambua, huamisha machungu au lawama kutoka kwa mwenye nguvu kwenda kwa mtu dhaifu. Hii hufanyika ili kuiridhisha nafsi au kujitetea kwa wakubwa.
Hivyo basi, polisi "wahalifu" wa Tanzania wameshindwa kushughulikia na wahalifu wakubwa, kwa kuwa wanawaogopa, na kuwabambikia dhaifu (wakiwemo watoto, maskini wasiohusika n.k.
Ndio maana wadau wanapendekeza mabadiliko makubwa ndani ya Jeshi la Polisi.
 
Hivi hakuna sheria ya kuwashitaki polisi na waendesha mashitaka kwa kukubambikia makosa? maana sasa ni too much unanikamata, unanitesa, unaniweka rumande, unananishitaki, mahakama inaniachia huru, na wewe unaendelea kudunda kitaa? this is absolutely unfair.....
 
OCD wa huko si ndio karudishwa Makao Makuu kwa sababu alipigiwa simu na wakubwa wake simu ikawa haipatikani kwa vile hakuichaji?

30th April 2013
Email
Print


Vurugu za kuchomeana nyumba zilizowakumba wakazi wa Wilaya ya Liwale, zimemtoa kafara aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo (OCD), Lucian Ngoromela, habari zikisema kuwa ameng'olewa na kurudishwa makao makuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi.


Mbali na hatua hiyo, kuna madai kuwa huenda akahojiwa ili aeleze kwa nini athari za tukio hilo zimekuwa kubwa kiasi hicho.


Hatua ya kumuondoa OCD Ngoromela Liwale imechukuliwa baada ya kubainika kuwa siku ya tukio (usiku wa kuamkia Aprili 24, mwaka huu), simu yake ya mkononi haikupatikana hadi kesho yake, kitendo ambacho kinadaiwa kilitoa mwanya kwa wahalifu kuchoma nyumba 20 ikiwamo ofisi ya serikali iliyokuwa ikitumiwa na Mbunge wa Liwale, Faith Mitambo (CCM).


Mbali na nyumba hizo, katika tukio hilo pia maduka 11 yalivunjwa na mali kuporwa huku trekta ndogo tano aina ya Powertiller zikiteketezwa kwa moto.


Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE lililokuwa limepiga kambi mjini humo, unaonyesha kuwa hatua ya kumng'oa OCD Ngoromela inalenga kurudisha imani ya wananchi wa wilaya hiyo kwa Jeshi la Polisi.


Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kikao cha pamoja kati ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, George Mwakajinga; Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Abdallah Ulega; Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Ephreim Mbaga na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mungulu.


Uchunguzi umeonyesha kuwa, wavamizi walianza kuchoma nyumba ya mbunge iliyopo kijiji cha Kingolowira Kata ya Nangando saa 2:30 usiku na waliendelea hadi alfajiri ya Aprili 24 bila hatua zozote kuchukuliwa na Jeshi la Polisi.


Habari zinasema kuwa wachomaji hao walikuwa wakisikika wakisema ‘tukimaliza kuchoma nyumba hii twende katika nyumba ya fulani' na kwamba walifanya hivyo.


Uchunguzi unaonyesha kuwa kukosekana kwa mawasiliano kulisababisha polisi kurundikana kituo cha polisi ili kulinda fedha zilizowasilishwa hapo na viongozi wa vyama vya ushirika baada ya wakulima wa korosho kukataa kupokea malipo ya nyongeza ya Sh. 200 badala ya Sh. 600 yaliyoahidiwa kutolewa awali.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Abdallah Ulega, alipoulizwa na NIPASHE kuhusu taarifa za uhamisho wa ghafla wa OCD Ngoromela, alithibitisha na kusisitiza kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kwa nia njema ikiwamo kutafuta amani ya kudumu wilayani humo.


Mapema akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa mji wa Liwale, Ulega alisema pamoja na kasoro mbalimbali zilizobainika katika mfumo wa stakabadhi ghalani, pia uasi umechangiwa na baadhi ya viongozi wa serikali kushindwa kuwajibika kwa wakati.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mwakajinga, alithibitisha kwa kuwa OCD Ngoromela, amehamishiwa makao makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi.

SOURCE: NIPASHE
 

hapo kwenye red sijaelewa chama gani sasa CCM au?
 
Hapo kwenye red, mkuu tujulishe upya. Kuona pia ni kosa?
 
Tuache kukurupuka watoto wa siku hz ni wadogo kwa umri., ila ni majambazi hatari.....
 
Mapolisi huwa yananiudhi jinsi yanavyokurupukaga kufuatilia kesi.,yanakamata watu na kunyanyasa watu hovyo bila hata kuwa na uhakika kama huyo mtu alihusika ktk tukio husika, Shame on them.
 
ipo kaka inaitwa malicious prosecution...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…