LIWALO NA LIWE WABUNGE WA BMK kupitia CCM si SHWARI TENA.

LIWALO NA LIWE WABUNGE WA BMK kupitia CCM si SHWARI TENA.

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,750
Nimepata faraja baada ya kuambiwa kuwa habari ndani ya CCM si shwari tena huko DODOMA ,wengi wa wabunge wa CCM walitaka kura iwe ya siri ,lakini kutokana na nguvu za wakubwa ambao ni vigogo wa CCM na viongozi waandamizi wa Chama hicho wamewataka waunge mkono msimamo wa kura ya wazi ,jambo ambalo limeigawa CCM.

Baadhi ya wabunge wa CCM wenye msimamo wa kura ya siri wamesema haburuzwi tena mtu ,siku za kutishana zimepitwa na wakati watamwaga razi hapohapo kwenye kura za wazi na liwalo na liwe na WaTanzania watajua na kusikia kuwa hakuogopwa Mwenyekiti wala mwenye meza wa CCM na wala hakuogopwa Katibu Kata wala Katibu Mtungi wa CCM ,wataelemea kule ambako WaTanganyika na WaZanzibari wanamatumaini napo na ndio maamuzi ya wananchi walio wengi.

Mambo ya kuogopana sasa hayana tena nafasi,wanalazimisha iwepo kura ya wazi ili waorodheshe majina yetu kuwa hatukuwaunga mkono na kwa vile wao ndio wenye Chama watatushughulikia ,safari hii tutashughulikiana na tutawaachia Chama Chao ,maana kuwepo kwao kunatokana na sisi kuwa pamoja nao ila tukianza kuwaachia kwa kuwa wao ndio wapo juu ya sheria basi wajue sio kuanguka bali watavunjika kabla ya kuanguka ,alisikika mbunge mmoja akielezea kama aliepoteza akili.
 
Hata hao wanaotaka kura ya siri ukichanganya wabunge wa upinzan na wa ccm bado hata robo hawajawafkia hao mamruk wanotaka kura ya waz
 
Sio sahihi Chama chochote kumshughulikia Mbunge,mbunge ni wa wananchi hasa kwenye mchakato muhimu kama huu.
 
Hili la katiba ni suala muhimu sana., kama mkifukuzwa uwanachama hakuna neno sis tutawamwagia mauwa kwenye hayo hayo majimbo yenu kupitia chama chengine tutawapokea kwa mikono miwili na heshma kubwa., waache CCM wajichanganye tu
 
Ccm sera kwishney imebak na sare mambo ya jf


Sent from my iPhone 5 using JamiiForums
 
Safi sana wenye msimamo msikubali kuburuzwa waigeni cuf na cdm pia nccr wameonyesha wazi wapo kwa ajiri ya wananchi na si chama
 
Hawana ubavu wa kupambana na nguvu ya chama!!watanzania sisi ni waoga ajabu!!!!kama sendeka anamtikisa waziri mkuu unategemea nini!!?
 
Wanaotaka kura ya siri CCM wanafiki kama wajanja si waoneshe msimamo wao hadharani na wawe tayari kutema ubunge kama chama kitawafukuza. Hapo watapata ujiko. Nasema wanafiki kwani Tanganyika wanaitaka na ubunge pia! Wachague moja!!
 
Back
Top Bottom