VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Aliyekuwa Mkrugenzi wa Utawala wa BOT,Amatus Liyumba, amedai kuwa kesi inayomkabili ya kukutwa na simu gerezani ni ya kupikwa na kubambikiwa. Akijitetea mbele ya Hakimu Mkazi Augusta Mmbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Liyumba amesema kuwa kesi hiyo ni uzushi mtupu.
Liyumba,akioongozwa na Wakili wake, alisema kuwa simu husika ililetwa na Maaskari wa Magereza na kamwe hajaingia nayo gerezani. 'Walikuja nayo askari magereza na kuanza kuniuliza mimi nimeipata wapi simu husika. Nasema simu yenye line nambari 0653004662 si yangu na siijui. Nimetengenezewa na kubambikiwa kesi hii' alisema Liyumba chini ya kiapo.
'Kwakuwa simu husika imesajiliwa,basi mmiliki atappatikana tu' aliongeza Liyumba. Hatahivyo, hakuna taarifa za kusajiliwa kwa nambari husika. Liyumba amemaliza kujitetea na hana shahidi mwingine wa upande wake wa utetezi.
Kesi husika ya kukutwa na simu inayomkabili Liyumba ni ya Julai 2011. Imeahirishwa hadi tarehe 5/1/2014 ambapo Mahakama itatoa hukumu.Pande husika za kesi hiyo zimetakiwa kuwasilisha hoja za majumuisho hadi kufikia tarehe 30/12/2013.
Chanzo: Mimi mwenyewe niliyekuwepo Mahakamani Kisutu juzi
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam