Local steaming!

Makuku Rey

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
3,497
Reaction score
3,823
kwa warembo wa jf naomba mnieleke namna ya kufanya steaming kwa njia ya kienyeji bila kutumia yale makemikali!

msaada tafadhali,nataka nimpendezeshe wifi yenu naturally.
 
mwambie atumie yai na parachichi iko poa kichizi... anaweza changanya na kahawa asilia na asali pia hii nimeambiwa leo
 
Mayonise changanya na mafuta ya olive pia nzur kwa nywele
 
QUOTE="Heaven on Earth, post: 18859880, member: 132738"]mwambie atumie yai na parachichi iko poa kichizi... anaweza changanya na kahawa asilia na asali pia hii nimeambiwa leo[/QUOTE]
Ni kweli kabisa, yai la kienyeji, asali mbichi, parachichi na tangawizi changanya vyote pamoja. Yaani mimi ndo naenda fanya sasa hivi. Hata kahawa asili nilishashuhudia mtu wangu wa karibu akifanyia.
 
mwambie atumie yai na parachichi iko poa kichizi... anaweza changanya na kahawa asilia na asali pia hii nimeambiwa leo
yai na parachichi au maharage achemshe yale maji yake pia unaweza kuchemsha mchele ukichemka nao maji yake yale pia majani ya mpera nayo kiboko
 
Japo Mimi sio mrembo, ilanaweza nikachangia kidogo... Sio kila steaming inaendana nanywele zako. Vile nywele zimetofautiana na steaming, lazima zitofautiane kulingana na aina, yanywele. Hatakama ni local steaming. Hadi madawa niivo ivo, mafuta ndokabisa.
 
Deep condition na shear butter cream.
 
Ukihitaji nywele ziwe nzito tumia parachichi na yai aisee hutajutia....
Pia waweza tumia tangawizi ukachanganya na mafuta ya nazi au olive oile......
Pia kuna majani ya mpera chemsha then paka kichwani....
Asali na yai.....
 
Mi nywele zangu ni nying na nzito .....tatizo ni kavu sanaaa .
Je, steaming itanifaaa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…