Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Kirusi kipya cha Omicron kilisababisha ongezeko la maambukiziImage caption: Kirusi kipya cha Omicron kilisababisha ongezeko la maambukizi
Kituo cha uchibiti na kuzuwia magonjwa cha Afrika (Africa CDC), kimesema sheria kali ya kukaa nyumbani au ‘lockdown’ sio tena njia bora ya kukabiliana na mawimbi ya virusi vya corona
Serikali sasa zinahimizwa kutumia hatua za afya ya umma na kijamii kupunguza viwango vya maambukizo ya virusi. Msisitizo wa chanjo kama hatua ya kukabiliana na virusi pia ulitolewa katika taarifa ya hivi punde wa CDC Afrika.
Nchi kadhaa zilikabiliwa na wimbi jipya la virusi kuelekea mwisho wa mwaka jana. Afrika Kusini ilihusisha kuongezeka kwa idadi yake ya maambukizi na kirusi kipya cha Omicron.
BBC Swahili
Mataifa kadhaa ya kusini mwa Afrika yaliwekewa marufuku ya usafiri kwa sababu ya kirusi hicho.