Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,299
Jamani sasa tunapokwenda sasa ni pabaya kuhusiana na hili sakata la kwenda kule Loliondo kupata kikombe cha Babu! Juzi nimeshuhudia mwenyewe hapa Arusha sasa hivi limeibuka sakata kati ya wanaojiita Sumatra/Trafick na wenye magari yanayokwenda Loliondo kupata kikombe cha Babu. kinachojiri hapa Arusha sasa hivi na nimeshuhudia kwa macho yangu wakati gari langu limekodishwa na watu waliokua wanakwenda Loliondo kwa Babu kupata kikombe, magari yamesimamishwa hadi pale tupate kibali ambacho wao wanadai kua tulipe Sumatra shilingi 9500 halafu baada ya hapo unatakiwa umuone vehicle inspecta akague gari naye anadai ni shilingi 10000 isitoshe mpaka huo mlolongo uishe iliupate hiyo Sumatra toa tena kitu kidogo kama shilingi 5000 sivyo utazungushwa ikiwezekana utalala bila kuondoka! jamani huu si wizi jamani? mwenye kutoa dawa yeye anatoza shilingi 500 yaani mia mbili za kanisa 200 za wafanyakazi wake halafu shilingi 100 ni ya Babu mwenyewe jamani tunakwenda wapi???? huu ni wizi? eti vehicle naye anakuzungusha na kukuambia gari lako halipigi honi kweli sasa imefika ule wakati wa mwananchi kujilipua kwa upuuzi kama huu na pia nahisi hata Babu kule Loliondo hajui hili jamani nawasilisha!