Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
* Hamad Rashid apigwa butwaa
Katika hali ya kushangaza, aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Salum Londa, jana aliwagawa waumini wa dini ya Kiislamu, baada ya kupiga kampeni msikitini akiwataka waumini hao wamchague mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete.
Londa alitoa kauli hiyo mara baada ya kukaribishwa katika ibada ya sherehe za Idd el Fitr iliyofanyika katika Msikiti wa Al farouq, Kinondoni, Dar es Salaa na kusisitiza Waisilamu kutofanya makosa kwa kupigia kura, kama walivyofanya mwaka 2005.
Londa amabaye alikuwa mgeni rasmi katika swala hiyo, alisema ipo haja ya Waisilamu kutofanya makosa na wajue umuhimu wa kuchagua viongozi kama miaka yote iliyopita.
Baada ya kutoa kauli hiyo, kundi la Waisilamu lilinyanyuka na kuondoka huku wengine wakilalamika kitendo hicho na kusema hakiendani na utamaduni wao kutumia nyumba za ibada kufanya kampeni za uychaguzi kwa viongozi wa siasa ...
.Akizungumza na Tanzania Daima mara baada ya kumalizika hotuba hiyo, Mbunge wa Wawi (CUF) amabaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni anayemaliza muda wake, hamad Rashid alisema hakupendezwa na kitendo cha kiongozi wa siasa kupiga kampeni msikitini, kwani kufanya hivyo ni kuharibu utaratibi katika nyumba za ibada.
Mimi nilipigwa na butwaa kwa kitendo hiki, kitendo cha mwanasiasa kusimama kwenye nyumba za ibada kumpigia kampeni mgombea fulani, kamwe hakikubaliki, alisema Hamad.
Wana JF: Hiyo ni sehemu tu ya stori ukurasa wa mbele katika Tanzania Daima ya leo.