London: Alazwa akiwa Ajitambui, Aamka akiongea kiitaliano

London: Alazwa akiwa Ajitambui, Aamka akiongea kiitaliano

Bakalalwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
748
Reaction score
1,217
Mwanamke mmoja aitwaye Althia Bryden kutoka London Nchini Uingereza ambaye alikua hawezi kuzungumza kwa miezi kadhaa kutokana na kupooza, ameripotiwa kuzinduka akiwa anazungumza lafudhi ya Kiitaliano licha ya kwamba hajawahi kutembelea Italia wala kujifunza lugha hiyo, mtandao wa Telegraph umeripoti.

Bryden mwenye umri wa miaka 58 aliugua kiharusi na kukimbizwa hospitalini mwezi wa tano mwaka huu ambapo alikaa Hospitalini kwa miezi kadhaa akiwa hawezi kuzungumza kabla ya kuamka akiwa anazungumza kwa lafudhi ya Kiitaliano tofauti na lugha yake ya Kingereza.

Bado haijajulikana chanzo cha hali hiyo lakini inadhaniwa kuwa Mwanamke huyo ana ugonjwa wa lafundi ya kigeni ambayo ni hali ya kiafya isiyo ya kawaida inayosababisha usemi wa Mtu kusikika kana kwamba ana lafudhi ya kigeni hata kama hajaipata au kujifunza lugha husika.

“Kadiri siku zilivyosonga ilikuwa wazi kwamba nilikuwa na lafudhi kali ya Kiitaliano na sikuwa na udhibiti wa sauti niliyokuwa nikizungumza wakati wa kuzungumza, kwa mshangao ninaweza pia kuzungumza Kiitaliano...lugha ambayo sijawahi kujifunza au kuzungumza hapo awali.” Amesema Bryden wakati akisimulia mkasa huo. #MillardAyoUPDATES
1735067319241.jpg
 
Back
Top Bottom