Lakini walipewa miezi sita na Border Agency kusafisha kati ya wale wanafunzi wanaohudhuria na kufuata masharti ya viza na wale ambao hawajawahi hata kutia mguu chuoni hapo ingawa wamesaidiwa na chuo hicho kuingia UK.
Na pia kuna wale ambao hawakuwa na viza kabisa na walikuwa wakisoma hapo bila kufuatiliwa uhalali wa makaratasi yao na hawa idadi yao inafikia 3000.
Sasa hili kundi la pili la wasio na karatasi ndilo linafuatiliwa maana ni kubwa mno na hata kama walikuwa wakiingia darasani lakini ni kipindi kimoja tu kwa wiki. Na hiki chuo kimeshindwa kufuata masharti hayo waliyopewa na UKBA.
Tatizo ni kwamba hii serikali inafanya mambo yake kisiasa mno bila kufuatilia kwa undani idadi ya wale wanaotoka nje ya Ulaya na kujua idadi yao bila kujumuisha wanafunzi.
Pia kuna vita kati ya vyuo kwa vyuo kwani London Met ni maarufu sana kwa kutoza ada inayoeleweka na sio kama kwa mfano ukitaka kwenda City University au Pale LSE.