Lonja Maana yake ni nini?

Lonja Maana yake ni nini?

Tman900

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
589
Reaction score
1,897
Leo katika Harakati zangu za Maisha Niko kwenye kiduka changu uchwala wamekuja wateja ktk maongezi yao wakataja neno Lonja nikajiuliza hili neno ni la kilugha au kiswahili na lina maana Gani.
 
Lugha ya jeshini maana yake ni tetesi ya kitu fulani karibu jeshini uliza na maana ya nanga
Unajua ktk Maisha Kila mtu Kuna kazi au maeneo anayopenda kutembelea. mi Binafsi maeneo ya Jeshi au Polis au Hospital za Jeshi sio mpenzi wa hayo Maeneo.
Pia kazi siko Interested na kazi ya Jeshi Wala polisi au Hata kua Mgambo
 
Toa mgambo apo huyo sio askari, njoo upige tizi utoe kitambi unyooshe mwili u feel mwili kulala hoi hae ujue uzalendo wa inchi yako.
 
Toa mgambo apo huyo sio askari, njoo upige tizi utoe kitambi unyooshe mwili u feel mwili kulala hoi hae ujue uzalendo wa inchi yako.
Maisha Kila mtu afanye apendacho Mimi napenda Biashara ndomana siku soma, mi nauza napata pesa, Basi ndo kazi naipenda hiyo Ya Jeshi lolote Kwenye nafsi yangu Wala haipo.
 
Toa mgambo apo huyo sio askari, njoo upige tizi utoe kitambi unyooshe mwili u feel mwili kulala hoi hae ujue uzalendo wa inchi yako.
Maisha Kila mtu afanye apendacho Mimi napenda Biashara ndomana siku soma, mi nauza napata pesa, Basi ndo kazi naipenda hiyo Ya Jeshi lolote Kwenye nafsi yangu Wala haipo
 
Tafsida za kijeshi hizo,ni sawa mtu akuambie wewe ni nanga.
 
Lonja ni msamiati ambao hutumiwa na askari & maafisa jeshini. Lonja limetokana na neno la kingereza “Launcher” likiwa na maana ya KIZINDUA.

Askari wa mizinga(ya masafa mafupi na marefu) hutegemea taarifa sahihi katika kupiga lengo(target). Grid Azimuths(Reference Point) za adui alipo na majeshi rafiki hutumwa kwa usahihi ili kuepusha madhara kwa majeshi rafiki. GA/RP husika hutumwa na askari wa miguu walioko uwanja wa mapigano(zero line).

Hivyo, neno lonja linapotumika na askari katika kipindi cha amani humaanisha “Tetesi/taarifa juu ya jambo fulani ambazo hazijathibitishwa na wakuu mbalimbali”.
 
Kwani zile nguo za bei rahisi zaidi pale kwenye maduka ya Kariakoo Dar uwa zinaitwaje vile? Siyo lonja?
 
PIa jeshini wakati wa gwaride maafande uwa wanapenda kutamka neno "kabalufu* kawataka maaskari wajipange vizuri kwenye mstari basipo kuacha nafasi kubwa kati ya askari na askari. Ninachojua hiyo "kabalufu" inatokana na maneno mawili ya kiingereza na neno la kwanza linaanza na "c" na la pili ni aloof. Hilo neno la kwanza ndiyo limenitoka naomba mwenye kujua anikumbushe.
 
Hujui maana ya" lonja"?
Sikiliza Wakongomani.
Lonja ni onja.
Kukatala M23 wasiingie Bukavu,maana yake kukataa M23 wasiingie Bukavu.
 
Back
Top Bottom