Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Kiwavi ni hatua ya ukuaji wa oda ya lepidoptera (wadudu kama vipepeo na nondo) ambao hutegemea majani kama chanzo kikuu cha chakula.
Hii ni hatua ya pili kwa ukuaji baada ya yai ambayo kwa baadae hugeuka kuwa bundo kisha mdudu kamili (kipepeo) ambaye huanza tena kutaga mayai mengine ili kuendeleza uhai.
Lonomia obliqua anayepatikana bara la America ya kusini ni kiwavi anayetoa sumu kali zaidi kuliko aina zingine zote za viwavi, hii ni kwa mujibu wa Guinness World Records (2016)
Historia
Nchi za Brazil, Uruguay, Paraguay, na Argentina ndiyo zinazotambulika kwa kuwa na aina hii ya kiwavi.
Visa vya kwanza kabisa kuhusisha viwavi hawa vilielezewa na Zoroastro Alvarenga mwaka 1912, lakini utafiti mkubwa Zaidi ulifanywa mwaka 1967.Kati ya mwaka 1989 na 2001, jumla ya visa 5673 na vifo 21 viliripotiwa kutokea nchini Brazil.
Viwavi hawa hutoa sumu inayo poozesha mfumo unaoongoza kuganda kwa damu mwilini.Aidha, huathiri figo, kuvujia kwa damu kwenye ubongo pamoja na kusababisha muwasho wa ngozi, maumivu makali ya kichwa, kutapika, kukojoa damu pamoja na wekundu wa Ngozi.
Kuvujia kwa damu kwenye ubongo pamoja na kushindwa kufanya kazi kwa viungo muhimu vya mwili ndiyo sababu kuu ya kifo.
Mambo ya ziada

- Mdudu kamili aliyekomaa huwa hana madhara yoyote kwa afya
- Kiwavi mmoja anaweza kutoa sumu inayofikia kiasi cha 2.4 mg
- Brazil ndiyo nchi yenye visa vingi zaidi vilivyowahi kuripotiwa
- Ukubwa wa madhara yake hutokana na kiasi cha sumu iliyoingia mwilini, inaweza kuonekana moja kwa moja au baada ya siku kadhaa
- Hakuna uhakika kwa tiba hasa kwa watu wanaokawia kwenda hospitalini