Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Lord Dalemera ni mtoto wa 2nd Lord Delemera. Alizaliwa Cheshire Uingereza 28 April 1870 na alifariki 13 November, 1931.
Lord Dalemera alisoma Eton na kumaliza shule akiwa na umri wa miaka 16. Kama kawaida ya watoto wa matajiri, ilikuwa kwenye mafunzo ya uafisa wa jeshi baada ya shule. Bahati mbaya Baba yake alifariki hivyo ilibidi asimikwe cheo cha baba yake akiwa na umri wa miaka 17.
Mwaka 1891 Lord Delemamera alifunga safari ya kwenda kuwinda simba huko British Somali Land. Katika uwindaji huo alikutana na Msomali mwenye bunduki aliyeitwa Abdullah Ashur. Ashur alimpa kipigo Lord Delemera kilichopelekea kuchechemea mpaka anaingia kaburini.
Lord Delamera alipata hati ya umiliki wa ekari 100,000 sawa na (400 km2) kwa miaka 99. Kwa makubaliano ya kulipa kodi ya £200 kwa mwaka na kutumia £5,000 kuendeleza eneo katika miaka mitano ya kwanza. Eneo alilopewa ni eneo la Naivasha.