Inaonekana ni 'Clip' ya karibuni ndani ya Onyesho la kimataifa la SAUTI ZA BUSARA, Zanzibar.
TUKIO:
Mtangazaji anamsogolea mkongwe, Mwana-HIPHOP-Mahiri, 'Mweusiiii' Lord Eyez. Huku onyesho likiwa linaendelea Stejini na anamdodosa 'Lord Eezy' maoni yake kwa Msanii mwenzake aliyeko stejini wakati huo 'bwana Ushauri' kama alivyombatiza kwa wakati ule 'rapa' WAKAZI.
Jibu la Lord limenifikirisha sana;
"Hata '94 tulikuwa hat-rap hivi na Cheko juu"
Ni Mara chache sana kwa Wasanii kupondeana hadharani hata kama wanayo yao wasiyokubaliana nyuma ya Pazia.
Lakini kauli 'kavu' ya Lord inashangaza. Sitaki kuamini kuwa yale ni maneno ya 'Kilaji' sababu mtoa kauli anaone kana kushikilia 'Bilauri', kilichomo ndaniyake wewe na mimi hatujui na si kazi yetu kujua. Tunaweza tukachuma dhambi kwani huenda ni 'Sharbat' tu ama lah ingawa ikiwa lah inaweza kuwa shida kidogo.
Yaani anamaanisha WAKAZI Hajapevuka Kisanii (Kwenye Ku-Rap) na hadi sasa yupo na 'staili' za nyuma kiasi kwamba ni zile za kukimbizana na akina Saleh Jabir, SOS B, Fresh G, Eazy B ama KU Crew ya Enzi za akina OJ nk?
Sikuwepo kwenye Tukio hivyo siwezi kuwa Pilato mzuri kuhukumu ubora na utendaji wa 'Wa-Job' pale.
Hatahivyo, kwa Heshma aliyonayo Eezy ktk tasnia ya Hip-hop mawili; Pengine Wana Maugomvi binafsi au tena ni kweli na hakika kwamba Kazi ya Wakazi ' YAKIDWANZI'.
Lord Eyes miaka Ile ya 2000-2009 alitisha Sana michano yake ilikua ina-sound like katoka Mambele.
Pia alikua na chemistry nzuri Sana na Ibra da hustler.
Ukiangalia Ngoma kama Ndo zetu kuwakilisha, Machafuko, Hawatuwezi, Ngoma zetu, tuna-bang, Niko ndani ya club na we ndo mchizi wangu zilikua hot sana hakika hakujawahi tokea kundi bora la hiphop hapa bongo kama Nako 2 Nako soldiers.
Rapper kutokea kundi la Weusi Lord Eyez, ameonyesha dhahiri kutovutiwa na mziki wa Wakazi na kumchana kuwa hajui kurap.
Your browser is not able to display this video.
Kwa upande mwengine, Show ya Wakazi hapo jana kwenye Sauti za Busara huko Zanzibar ilikatishwa ghafla baada ya kukaa kwenye stage kwa dakika 2 tu. Kabla ya kuondoka jukwaani Wakazi alisikika akisema “kuna watu wanatubania aisee”. Wapenzi wa Hip Hop huko Zanzibar pia hawakufurahishwa na tukio hilo.
Lord Eyes miaka Ile ya 2000-2009 alitisha Sana michano yake ilikua ina-sound like katoka Mambele...
Pia alikua na chemistry nzuri Sana na Ibra da hustler...
Ukiangalia Ngoma kama Ndo zetu kuwakilisha, Machafuko, Hawatuwezi, Ngoma zetu, tuna-bang, Niko ndani ya club na we ndo mchizi wangu zilikua hot sana hakika hakujawahi tokea kundi bora la hiphop hapa bongo kama Nako 2 Nako soldiers...
mwandishi ndo alikuwa anatafuta namna ya kuonesha wakaz kiwango kidogo, maana kila lord eyes akikwepa kumponda wakaz, mwandishi analazimisha ionekane kama kuna viwango wakaz hana ili eyez amchane, all in all wakaz naye miyeyusho , kudis wenzake na kujiona bora "bwana ushauri"
mwandishi ndo alikuwa anatafuta namna ya kuonesha wakaz kiwango kidogo, maana kila lord eyes akikwepa kumponda wakaz, mwandishi analazimisha ionekane kama kuna viwango wakaz hana ili eyez amchane, all in all wakaz naye miyeyusho , kudis wenzake na kujiona bora "bwana ushauri"