Lori la Mizigo Lapinduka Tanga, 3 Wafariki, 7 Wajeruhiwa

Nyundo_tz

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2009
Posts
640
Reaction score
20
Lori la Mizigo Lapinduka Tanga, 3 Wafariki, 7 Wajeruhiwa
3171562.jpg

Thursday, September 24, 2009 10:21 AM
WATU watatu wamekufa papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya baada ya lori la mizigo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka huko Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.Ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 9:45 jioni katika barabara ya Dindira Wilayani Korogwe.

Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Mistubishi Fuso lenye namba za usajili T 900 AWK lililokuwa likiendeshwa na Cuthbet Mzinga (30).

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Simon Mgawe, alitoa taarifa hiyo na kusema kuwa lori hilo lililokuwa likitokea Kijiji cha Mali kuelekea mji wa Korogwe, liliacha njia na kugonga kalavati na kisha kupindukia bondeni mwa barabara hiyo umbali wa mita 60.

Amesema watu waliopotezad maisha paohapo walifika watatu wengine saba alijeruhiwa vibaya ambao wamekimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe ya Magunga kwa matibabu

Kamanda Mgawe aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Nuru Ali (25), Dustan Andrew (45), Haruna Amiri (25), Amiri Salim (25), Idrisa Rashid (32), Ali Hassan (49) na Abiud Makai (32) na majina ya marehemu hayo hayakupatikana mara moja wakati habari inachukuliwa.

Thursday, September 24, 2009 10:21 AM
WATU watatu wamekufa papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya baada ya lori la mizigo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka huko Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 9:45 jioni katika barabara ya Dindira Wilayani Korogwe.

Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Mistubishi Fuso lenye namba za usajili T 900 AWK lililokuwa likiendeshwa na Cuthbet Mzinga (30).

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Simon Mgawe, alitoa taarifa hiyo na kusema kuwa lori hilo lililokuwa likitokea Kijiji cha Mali kuelekea mji wa Korogwe, liliacha njia na kugonga kalavati na kisha kupindukia bondeni mwa barabara hiyo umbali wa mita 60.

Amesema watu waliopotezad maisha paohapo walifika watatu wengine saba alijeruhiwa vibaya ambao wamekimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe ya Magunga kwa matibabu

Kamanda Mgawe aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Nuru Ali (25), Dustan Andrew (45), Haruna Amiri (25), Amiri Salim (25), Idrisa Rashid (32), Ali Hassan (49) na Abiud Makai (32) na majina ya marehemu hayo hayakupatikana mara moja wakati habari inachukuliwa.

</SPAN>
 
Back
Top Bottom