Lori lagonga daladala Mwenge mataa, watu watano wanadaiwa kujeruhiwa
Mapema leo mida ya Saa 12 asubuhi EATV imepokea taarifa ya kutokea kwa ajali ya gari kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Sam Nujoma, maeneo ya Mwenge Mataa ambapo Lori lililokuwa linatoka barabara ya Bagamoyo kuelekea Makumbusho linasemekana kuwa limegonga daladala inayofanya safari zake Makumbusho - Boko.
Shuhuda wa ajali hiyo ameeleza kwamba ajali imesababishwa na dereva wa Lori, kutokana na uharaka wake wa kuwahi safari zake, ingawa askari wa usalama barabarani alikuwa ameruhusu magari yanayotoka barabara ya Sam Nujoma kupita.
Mpaka EATV inapokea taarifa hizi imeripotiwa kuwa na majeruhi watano na hakuna vifokutokana na ajali hii.