Lori lagonga treni, foleni ndefu mataa ya Chang'ombe

Lori lagonga treni, foleni ndefu mataa ya Chang'ombe

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Lori aina ya fuso limegonga treni kwenye njia yake baada ya mataa ya Chang'ombe, Dar uelekeo wa Magomeni. Ajali hiyo imesababisha foleni barabara ya Nyerere kutoka mataa ya Veta Chang'ombe kuvuka daraja la Mfugale, Tazara. Pia imesababisha foleni Kubwa barabara ya Chang'ombe.

Watumiaji wa barabara wanashauriwa kutumia barabara mbadala. Juhudi za Kuondoa treni na lori katikati ya barabara zinaendelea.

IMG_20201020_073932_6.jpg
 
Lory linagongaje Train hii sheria ya mkoloni inahitaj marekebisho
Train zinapita bila kujali kabisa watumiaji wengine wabarabara au angalao kuwepo na kibendera kama ilivo mabibo...
Angalao kuwe hata na taa bas
Pole sana mwenye lory na dereva
 
Ndo maana barabara inayo cross railway inawekwa tahadhari kabisa kuashiria kwamba wewe unayetumia barabara ndiye unayepaswa kuwa makini na sio treni inayopita kwenye reli yake kwa sababu katika hali ya kawaida barabara ndio iliyokatiza relini na sio reli imekatiza barabarani.
Fuatilia kwa makini mzazi. tehe tehe tehe tehe
 
Lory linagongaje Train hii sheria ya mkoloni inahitaj marekebisho
Train zinapita bila kujali kabisa watumiaji wengine wabarabara au angalao kuwepo na kibendera kama ilivo mabibo...
Angalao kuwe hata na taa bas
Pole sana mwenye lory na dereva
Mkuu tatizo ni brake application ya hizo mambo siyo kama za magari hasa inapokuwa na mabehewa ni bora ikawa Locomotive pekee hapo kweli uzembe utakuwa kwa dereva wa treni pia. Ila ikiwa na mabehewa huwezi fanya brake application hapa usimame hapo hapo. Nadhani zuri zaidi wangeweka watu wa vibendera au yale mageti.
 
Kwani barabara ya magari ndio inakatisha kwny barabara ya treni au barabara ya treni ndio inakatisha kwny barabara ya magari?
Lory linagongaje Train hii sheria ya mkoloni inahitaj marekebisho
Train zinapita bila kujali kabisa watumiaji wengine wabarabara au angalao kuwepo na kibendera kama ilivo mabibo...
Angalao kuwe hata na taa bas
Pole sana mwenye lory na dereva
 
Lory linagongaje Train hii sheria ya mkoloni inahitaj marekebisho
Train zinapita bila kujali kabisa watumiaji wengine wabarabara au angalao kuwepo na kibendera kama ilivo mabibo...
Angalao kuwe hata na taa bas
Pole sana mwenye lory na dereva
Muda mwingine huwa wanakosea hao waongoza treni... unakuta treni inakaribia kwenye road cross... ndio honi inapigwa... tahadhari haitolewi mapema... kuna muda lazima usababishe ajali kutokana na hayo.
 
Lory linagongaje Train hii sheria ya mkoloni inahitaj marekebisho
Train zinapita bila kujali kabisa watumiaji wengine wabarabara au angalao kuwepo na kibendera kama ilivo mabibo...
Angalao kuwe hata na taa bas
Pole sana mwenye lory na dereva
Unapendekeza sheria iweje mkuu?

Karibu duniani kote matumizi ya barabara huzuiwa kwa muda (road blockage) kuipa treni kipaumbele.

Hii ina maana kwamba, kila kwenye makutano ya barabara na reli, treni ndiyo inayopewa kipaumbele.

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Vijana wa vyuo vya ufundi mfano pale DIT au ATC wameunda mfumo huo uliouweka hapo na niliwaoa 👊 kutokana na teknolojia yao maana haikuwa inataka mtu aiongoze ila...

Ilikuwa na signal ambapo train ikikaribia na barabara ya magari basi hizo road block zinajifunga zenyewe na zinatumia mfumo wa jua badala ya umeme.

Tatizo ni kwamba serikali zetu za kiafrika kama Tanzania hazina muda na vijana wetu kama hawa gata kuwapa nafasi kuunda hii mifumo ikatumika.

Wanasiasa waache kutudanganya kuwa treni haiwezi kuwa na makosa, tunahitaji vitu kama hivi kwenye vivuko vyote vya reli barabarani...View attachment 1605834
 
Lori aina ya fuso limegonga treni kwenye njia yake baada ya mataa ya Chang'ombe, Dar uelekeo wa Magomeni. Ajali hiyo imesababisha foleni barabara ya Nyerere kutoka mataa ya Veta Chang'ombe kuvuka daraja la Mfugale, Tazara. Pia imesababisha foleni Kubwa barabara ya Chang'ombe.

Watumiaji wa barabara wanashauriwa kutumia barabara mbadala. Juhudi za Kuondoa treni na lori katikati ya barabara zinaendelea.

View attachment 1605703
Kwanini hizi njia zisiwekwewe vizuizi vya kutumia umeme kama wenzetu ulaya, hapa kwetu ni kama tunazunguka kinyume cha mwendo wa saa
 
Lory linagongaje Train hii sheria ya mkoloni inahitaj marekebisho
Train zinapita bila kujali kabisa watumiaji wengine wabarabara au angalao kuwepo na kibendera kama ilivo mabibo...
Angalao kuwe hata na taa bas
Pole sana mwenye lory na dereva
Wabunge wenyewe wa kubadilisha hii Sheria ndio hawa wanaopiga magoti na kujigaragaza kwenye vumbi.
Tell me another one
 
unakuta mtu yupo feleni na gari yake kakaa kwenye reli badala ya kuacha nafasi. motokeo yake ndio hayo
 
This a hundred year old technology ndio muarobaini wa tatizo la hapo.
Wahisika wame-let the guard down and are totally responsible for the accident.
tapatalk_1603214155670.jpg
 
13 November 2022
Songwe, Tanzania

AJALI SONGWE, GARI LAGONGA TRENI LA MIZIGO, ABIRIA WANUSURIKA KIFO..

Abiria kadhaa wamenusurika kifo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria, lenye namba za usajili T388 DUS kuligonga treni la mizigo katika makutano ya Barabara Kuu ya Tanzania na Zambia (Tanzam) katika eneo la Songwe mkoani Songwe, tukio lililotokea jioni ya Novemba 13, 2022. Picha za video kutoka eneo la tukio, zinalionesha treni ya mizigo ikiwa imepinduka baadhi ya mabehewa na kufunga barabara hiyo
Source : Global TV Online
 
Back
Top Bottom