Love at first sight

Afu ukanidanganya wewe bado bikira...
 
Awwww. Hongera sana mama. Namna napenda mapenzi naelewa unavyojisikia moyoni. Mwenyezi Mungu awajaalie miaka mingi yenye furaha pamoja.
 
Joanah umenikumbusha mika mingi sana iliyopita,,ilikuwaje kwangu binti alikuja ofsin kuleta barua ya maombi ya kazi siku tu nimemuona alipoingia ofsini nikasema huyu ananifaa kuwa mke.
Nilimhoji vimaswali vya hapa na pale kutaka kujua machache nikamwambia maneno matatu tu, 'Nataka Mtoto Kwako'! basi hakunihoji wala nini akaondoka home kwao, basi bhana nikamwambia aje achukue majibu yake tarehe fulan moyoni nikijisemea hakuna majibu ya kazi hapa. Siku ikafika akaja kusikilizia majibu nilimweka kwny bench kunisubiri mpaka jioni ili tutoke pamoja, alikalia benchi huyoo mpaka akachoka wakat huo huo walikuwepo pia wengine nao walileta maombi ya kazi nikawa nawajibu haraka na kuondoka mlengwa yupo tu amekaa kwny bench. Muda wa kufunga ofisi ukafika nikamwita akaingia nikamwambia pole sana kwa kukaa muda mrefu kazi nyingi na mambo kama hayoo majibu yako ya kazi ni mazuri kwa hiyo tuondoke nyumbani muda ushakwisha, akaniuliza tunaenda wapi nikamjibu twende tukamuone mdogo wangu anaumwa halafu wewe utaondoka baadae kwenda nyumbani kwenu alikuwa anakaa kwa shangaz yake akakubali tukaondoka zetu haooo mpaka kwa dogo, bahati nzur tukamkuta alifurahi sana dogo kuona nimeenda kwake na mgeni muda huu saa 1 usiku na midakika kadhaa hivi,, dogo akatuacha kwa dakika chache kumbe kenda kununua mboga samaki na kuku waliokaangwa chakula kikaandaliwa tukala baada ya kumaliza kula dogo akasemaje mgeni tafadhali ingia bafuni nishakutengea maji ya kuoga ya moto akajaribu ka kugoma vile akidai anataka awahi home atachelewa sna dogo akamwambia nimefanya kwa heshima sio kwa ubaya wewe nenda kaoge taulo nishaweka lipo huko huko,hatimae akakubali akaenda kuoga muda huo saa ngap sasa likuwa mida ka saa 3 kuelekea mishale ya saa 4 hivi usiku,mm na dogo tukabaki tunachek tv dogo akaniambiaje brother nikwambie kitu ehhheee sema huyu ndiye mke wa kuoa!!!
Alivyotoka kuoga dogo akanigeuzia kibao mm akaniambia bro zamu yako nenda kaoge, wakat huo dogo kumbe keshaandaa room maalum kwa ajili kulala niliporudi tu kuoga dogo akaniambia ingia ndani brother mgeni yupo ndani anakusubir kuingia si nikamkuta amejifunika shuka tayar safar ya kwenda kwao kaogopa usiku mwing,,
Weee asikwambie mtu ukiwa umemfeel mtu aisee nilifanya mazito sana siku hiyo goooli 8 mpaka asubuh kumbe siku hiyo zilikuwa ni siku zake za kutunga mimba,,
Leo ni miaka 25 tupo ndani ya ndoa saaafi haina hata mgogoro na Mungu akatujalia watoto 4..maisha haya hayana fomyula ndugu zangu..
 
Ilitokea hii miaka 9 iliyopita yeye anasoma form six mi nipo chuo mwaka wa pili.mara ya kwanza namuona nkajisemea huyu ndo mwananke wa maisha yangu.nashkuru mungu now tupo kwenye ndoa mwaka 5 mungu ametubariki na mtoto mmoja.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mdogo wako mjanja sana
 
Jo huoni idadi ya nyuzi unazofunguliwa lakini...means you're adorable, yaani wapendwa/wavutia kama vile inavyopendwa chips mayai...
Amna kitu hapo,ungese mtupu

Sioni sababu ya kuanzisha uzi wakati kuna kitu inaitwa PM,mtu anayenianzishia uzi wa kudai ananipenda ni attention seeker tu...hakuna upendo hapo
 
[emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…