Love bite sehemu ya kwanza

Omaryjr1

Member
Joined
Jun 8, 2017
Posts
17
Reaction score
25
LOVE BITE
♥️🔥
SEHEMU YA KWANZA ( 01 )



Ni siku ya jumapili iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa watu kutoka sehemu mbali mbali walionekana kwenye kumbi za starehe.
Wengi ambao walikua wanapenda taarab basi walijazana travertine hotel kuwaangalia jahazi.
Kwa wengine wanaopenda bongo flavour basi walikutana bills,maisha,masai..Dar live na kumbi zingine zilikuwa na wasanii pendwa waliokuwa wanaburudisha week end hiyo.
JOTHAN alikua anapendelea sana mixing za ma dj mbali mbali. Hivyo jumapili hiyo aliamua kwenda coco beach usiku huo.
Upepo mwanana uliokuwa ukipuliza huko coco beach na ukichanganya na big screen iliyokuwa inaenda sambamba na mixing za maana alizokuwa anazipiga dj huyo aliyezikonga roho za watu wengi waliokuwa pale, iilikuwa burudani tosha kwa waliohudhuria usiku ule.
Jotham alipaki gari yake pembeni, alichagua kiti kilichukokuwa karibu na meza ya mwisho na kuagiza kinywaji alichokipendelea na kuendelea kufurahia mziki uliokuwa unaonyeshwa kwenye screen hiyo.

Mara kwa mara madada poa walikuwa wanajipitisha pale alipo, lakini aliwachora tu na hakuwa na mpango nao.
Baada ya dakika kadhaa, walitokea madada watatu waliokuwa wameingia pale coco beach na kuanza kutafuta mahali pa kukaa. Waliangaza meza nyingi zilikua na nafasi ya mtu mmoja au wawili tu na wao walikuwa na lengo la kukaa wote watatu kwenye meza moja.
Baada ya kuangaza kwa muda, waliiona meza aliyokaa Jothan ikiwa na nafasi tatu za kukaa. Waliisogelea ile meza na walipokaribia tu kuifikia ile meza. Walishuhudia jamaa mmoja akiwa ameenda kukaa pale.
“wewe kaka sogea sehemu yetu.” Aliongea mmoja kati ya wale wadada watatu baada tu ya kuifikia ile meza.
“mbona hakuna alama yoyote kuwa mlikaa hapa. Hakuna vinywaji wala kitu chochote.” Aliongea yule jamaa huku akionyesha wazi kuvutiwa na ile sehemu iliyokuwa chemba lakini ikiwa inaonyesha vizuri ile tv.
“ni vyema uwapishe kwa sababu waongeacho sio uongo.” Aliongea Jotham kumwambia yule jamaa. Hakuwa anapenda makelele ambayo alijua yatatokea baada ya mvutano huo wa kugombania ile sehemu.
Yule jamaa akaamua kunyanyuka na kuwapisha wale warembo na yeye kwenda kukaa meza nyingine.
“ahsante sana kaka, maana yule jamaa alitaka atubanie wakati sisi tumehangaika kutafuta meza tutakayokaa wote watatu”. Aliongea yule dada aliyeonekana kama kiongozi wao.
Mavazi waliyovaa yalitosha kumshawishi mvulana yeyote rijali na kufanya iwe lazima macho ya matamanio kumtoka.
Uzuri wa mabinti hao likuwa unashinda lakini huyo aliyekuwa kiongozi wao aliwazidi wenzake kwa kila kitu.
Macho ya Jotham yaliona kila kitu kutoka kwa binti huyo mbichi. Chuchu zilitokeza kwa kujichora kwenye gauni ile nyepesi ambayo haikuwa na nguo nyingine ndani.
“sikiliza oda zao, ziingize kwenye bili yangu” aliongea Jotham baada ya kumuita muhudumu aliyekuwa anamuhudumia toka afike pale.
“ahsante.” Waliitikia wale madada baada ya kupewa ofa hiyo.
Waliagiza vyakula na vinyaji walivyopendelea. Walipiga story za kawaida huku wakigongeana glass za vinywaji na kucheka.
Jotham alikuwa kimya wakati wote huku akiwa bize kuangalia na kusikiliza mixing ambazo ndizo zilizomleta pale.
Baada ya masaa kadhaa, alimuita muhudumu na kulipia bili yake.
“ahsante kwa ofa yako.” Aliongea yule kiongozi wao baada ya Jotham kuwaaga.
Jotham aliingia kwenye gari yake aina ya opah na kuondoka eneo hilo.
Njiani alimkumbuka yule dada lakini aliishia kucheka tu kwakua hakuwa na hisia zozote za mapenzi juu yake. Zaidi alimtamani kuwa nae japo kwa usiku mmoja kwa jinsi alivyotoka. Hakika alikuwa na kila aina ya uchochezi wa kufanya ngono.
Alifika kwake usiku mnene na kwenda kulala fofofo kutokana na usingizi uliojaa wakati huo.
Asubuhi aliamka na uchovu tele na kwenda kuoga ili kujaribu kuupunguza uchovu aliokuwa nao. Alipomaliza kuoga. Alijiandaa tayari kwa kwenda kazini.
Alisumbuka sana kuwasha gari lake lakini halikuwaka. Alipoangalia mafuta, aligundua kuwa wese lilikuwa limekata. Kwa kuhofia kuchelewa zaidi kazini, aliamua kwenda kituoni na kupanda daladala.
Alifika kazini huku macho yake yakiwa mekundu yaliyoashiria kuwa bado alikuwa na usingizi.
“mshikaji bora ukapate supu, maana hiyo harufu ya pombe uliyamka nayo ni noma. Utaongea vipi na bosi?” alishauri mmoja wa wafanyakazi wenzake aliyekuwa karibu naye.
“poa, ngoja nielekee canteen basi.”
Aliongea Jothan na kwenda canteen kupata supu ya mbuzi na chapati.
Baada ya kunywa chai, alirudi na kuendelea na kazi.
Saa nane ndio muda waliokuwa wanatoka kazini. Alienda kupata chakula cha mchana canteen na kuondoka zake kuelekea kituo cha daladala ambacho hakikuwa mbali na ofisini kwao.
Alisubiri daladala kwa muda na kupanda gari iliyokuwa inaelekea mwenge kwa malengo ya kushuka kinondoni anapoishi.
Usingizi ulichukua nafasi yake baada ya kupanda tu lile gari lililokuwa likisubiri abiria kwa dakika kadhaa pale kituoni
Baada ya muda mrefu kidogo kupita, aliamka na kuangalia gari lilikuwa limefika wapi. Wakati akiwa anaanga angaza, macho yake yaligongana na yule mrembo aliyekuwa naye kwenye meza moja siku ya jana yake. Wote walikumbukana na kila mmoja akamuachia mwenzake tabasamu.
Hapo alifanikiwa kumuona vizuri huyo msichana mwenye kila sifa ya uzuri.
Usingizi uliendelea kumzonga Jotham na kujikuta anapitiwa na usingizi bila kuongea chochote na yule msichana.
Gari lilifika mpaka mwenge na kupitiliza kituo alichokua anashuka Jothan. Aliamshwa na konda baada gari kushusha abiria wote.
“tuko wapi hapa.” Aliuliza Jothan baada ya kuamka na kuangalia nje ambapo kulikua tofauti na mazingira anayoishi.

“tumeshafika mwenge kaka.” Alijibu yule konda.
Jothan aliangalia huku na kule na hakuona abiria yeyote aliyekuwa kwenye lile gari zaidi yake.
Hakusikitika kupitishwa kituo, bali alisikitika sana kutochukua namba wala kujua jina la yule msichana aliyevutika naye zaidi baada ya kuonana nae kwa mara ya pili.

ITAENDELEA….
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…