Love Languages (Lugha za kimahaba)

Love Languages (Lugha za kimahaba)

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Je, wajua ni ipi lugha yako ya kimahaba?

Japo tunaweza kusema kuwa haya ni mambo ya wazungu. Lakini kihisia binadamu wote tupo sawa huku tukiwa na tofauti ndogo ndogo zinazotutofautisha na wengine.

Zipo lugha kadhaa zilizothibitishwa kutumika kati ya mtu mmoja na mwingine linapokuja suala la mahaba. Nazo ni kama ifuatavyo:

1. Maneno ya pongezi au sifa (Words of affirmation).
Wapo watu wanaopenda kusikia maneno mazuri mazuri muda wote ili wajisikie kupendwa, we wasifie tu utaona matokeo.

2. Muda mzuri kukaa pamoja (Quality Time).
Ukisikia kuna watu wanafungiwa ndani wasiende kazini ilimradi tu washinde pamoja ujue ndo hawa. Na zile za kupenda mitoko (outings)ili kufurahia muda mzuri wakiwa pekee yao bila bughudha.

3. Kukumbatiana (Physical Touch).
Hawa ni wale wanaosisimuliwa na miguso kutoka kwa wenza wao. Maneno buku bila kumgusa mwenzio ni kazi bure, hata wakiwa barabarani utaona wameshikana mikono huku wakitembea kwa raha zao.

4. Kusaidiana Kazi (Acts of service).
Hapa ni wale wa kupenda kusaidiwa kazi. Msaidie kubeba hata mkoba tu uone anavyofurahi, ukimsaidia kupika ama usafi wa nyumba utapewa hata vile hujawahi kupewa.

5. Kupokea Zawadi (Receiving Gifts).
Hili kundi limekuwa la mkumbo, wengi hata wale wasiojua wanahitaji nini wamekuwa wakijiunganisha na kundi hili kwa kuonesha wanapenda kupokea zawadi. Jukumu la kutoa hizo zawadi sijui wanamwachia nani.

Ni mara chache sana mtu mmoja kuwa kwenye makundi zaidi ya moja. Ila wengi wetu kwa kutokujua au kwa kujiongopea tunatamani kundi lisilo letu, ndiyo sababu hata hatujisikii kupendwa na wenza wetu kwa sababu hatujui ni kwa namna gani tunapaswa kuoneshwa upendo huo.

Hebu basi karibuni tutiririke lugha ya kila mmoja wetu hapa.

Karibuni.
 
Chakula utanunua na mawe?
kuna wakulima wamelima viazi mkuu na havihitaji chumvi ni kuchemsha tu unakula unashiba usikumbatie? kuna Watu wana migomba ya ndizi hao kuna hitaji la hela ili ashibe au hawapo kwenye kundi la kukumbatiana mpaka wawe na hela?
 
88B83534-A30A-4C32-8F70-6779C3F23019.jpeg
 
Back
Top Bottom