Wako wachache sana waliowahi kufanikiwa kwa njia hii na wengi wao kushindwa. Ila pia wapo ambao waliijaribu njia hii na kufanikiwa mpaka leo hii wameona hawana sababu tena ya kufunga ndoa, that is to say, wamejiona kama wamefunga ndoa tayari maana wameishi kwa miaka mingi pamoja na kuzaa watoto kiasi kwamba ndoa kwa sasa haina faida tena kwao.
Kwa hali ilivyo hivi sasa binafsi sirecommend hii njia. Kimsingi naona kama ina matatizo makubwa sana pale unapojaribu kujaribu kuishi na mtu na mkashindwa kuwa "compatible". Katika hali kama hii, ni rahisi kujikuta unaishi kinyumba na kila mwanaume na ikitokea kushindwana unapigwa chini. Ukishajaribu mchezo huu zaidi ya mara mbili, wanaume watakuona muhuni na suala la ndoa linaweza kuota mbawa kabisa.
Ni vzr kujiheshimu kwa kuishi kwako, then mkifunga ndoa mtajuana huko huko. Mambo mengi watu hufundishana ndani ya ndoa. Kikubwa ni kuwa na upendo na kukubali kusikilizana na kutumia busara kwenye maamuzi yenu ya kifamilia.
HP