Low cost greenhouse technology

manasem

Member
Joined
May 4, 2010
Posts
6
Reaction score
2
SHADENET GREENHOUSE: NJIA SAHIHI KATIKA MAFANIKIO YA KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA MATUNDA
•Ni shamba lililozungushiwa uzio wa net juu na pembeni.
•Ni jengo maalum ambalo ndani yake ni mahususi kwa kupandwa mazao (Kilimo)
•Ni jengo ambalo linamfanya mkulima kuwa na uwezo wa kuhodhi hali ya hewa kwa ajili ya mazao yake
•Kilimo cha Bustani yaani kilimo cha mbogamboga na matunda humu ndimo mahala pake haswaa!!!

KWANINI GREENHOUSE

•Kilimo kinakabiliwa na vihatarishi vikuu vinne ambavyo husababisha mavuno kuwa madogo.
1.Jua
2.Upepo
3.Wadudu
4.Matumizi sahihi ya maji
•Greenhouse huondoa ama huzuia vihatarishi hivi kuufanya mmea usifikie malengo yake ya kutoa mazao katika wakati muafaka, kiwango sahihi na ubora unaotakiwa.

UMUHIMU WA GREENHOUSE

1.Huwezesha mimea uzaa mapema nakuishi kwa muda mrefu zaidi tofauti na kilimo cha wazi

  • Mmea huzaa mapema e.g nyanya 2 months, hoho 2.5months
  • Mmea huweza kuishi muda mrefu e.g Nyanya 1yr, Hoho 6months, Swetmelon 5-6months, Tango 1yr.

2.Humuwezesha mkulima kuchagua aina nyingi za mazao anayotaka kulima wakati wowote ule

  • Mazao yoyote yaweza kuzalishwa katika greenhouse kwani hali ya hewa na aina ya udongo yaweza tengenezwa kulingana na mahitaji.

3.Hulinda mazao kushambuliwa na wadudu waharibifu
4.Matumizi madogo ya sumu

  • Kwakua magonjwa ya kuambukiwa yatakua yamedhibitiwa basi, matumizi ya dawa za sumu yatakua madogo sana ama hakuna.
  • Kwakua matumizi ya madawa yatakua madogo basi, mazao yatakayotoka yatakua almost ORGANIC.
5.Mazao bora na mengi hupatikana

  • Kwakua hali ya hewa ma mazingira ya uzalishaji yatakua yameboreshwa basi, mazao yatakayotoka yatakua yenye ubora wa hali ya juu.
6.Matumizi sahihi ya maji

  • Kwakua unyevu ndani ya shamba utakua unahifadhiwa , kwahiyo matumizi ya maji yatakua matuzi.
  • Kwakua kutakuwa na mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone, matumizi ya maji yatakua mazuri sana na gharama za uendeshaji zitapungua zitapungua
7.Huficha mazao yako mbali na majirani ama wapitanjia

  • Kutakua na usiri katika kuyakuza na kuyatunza mazao shambani kwani ni ukweli wapita njia na majirani sio wote wanaopenda maendeleo ya mtu.
8.Gharama za uendeshaji ni ndogo

9. Net huzuia:
a)Jua kuiumiza mimea (stress) hivyo kuifanya kutengeneza chakula chake katika hali tulivu
b)Jua kuikausha ardhi hivyo kuondoa upotevu wa maji ardhini kwa haraka
c)Upepo kuiumza mimea (stress)
d)Upepo kuleta magonjwa yanayosafirishwa na kuambukizwa kwa upepo
e)Wadudu waharibifu wa mazao na wanaoleta magonjwa.
f)Wanyama waharibifu kama panya na ndege


MFANO WA KILIMO CHENYE TIJA (HOHO)

•Gharama za uwekezaji – Jengo (18m by 8m) -3,200,000/=
•Gharama za uzalishaji – 1,800,000/=
•Mavuno yanayotarajiwa – 5,760,000/=
•Faida baada ya mavuno
1.Cash - 760,000/=
2.Jengo litalodumu sio chini ya miaka 5
•Muda wa kilimo – miezi 6

GHARAMA ZA UZALISHAJI
1.Mbegu – 60,000
2.Samadi – 100,000
3.Mbolea nyingine – 100,000
4.Madawa – 100,000
5.Mshahara wa Mfanyakazi – 480,000
6.Chakula cha mfanyakazi – 240,000
7.Umwagiliaji - 450,000
8.Solo – 250,000

MAVUNO
Muda mpaka kuanza kuvuna batch ya kwanza – miezi 3
Muda wa kuvuna mazao baada ya kuyakuza kwa miezi 3 – miezi 3 mingine (jumla 6months)
Miche shambani 480
Matunda @ 10 – 4800 kwa batch
Batch ktk 3months – 6
Bei ya tunda 200/=
Mapato ya batch – 960,000/=
Mapato ya miezi 3 ya mavuno – 5,760,000/=

MAWASILIANO
Ken Products Enterprises
Plot no.868 Block ‘E’ Tegeta
P.O Box 20600
Kinondoni
Dar es salaam
Tanzania
Tel:+255652402665
Mob:+255772668500
Email: kenproducts@gmail.com
 
Ndugu kwa uelewa wangu mdogo, nijuavyo mimi shed nets ni tofauti na greenhouse, green house asilimia 25 inakuwa ni karatasi maalum la nailon linaanzia juu kukinga mazao na jua na mvua na 75 asilimia ndiyo zinakuwa nets pia hutegemea eneo kama siyo baridi sana. Shed nets ni kwaajili ya kukinga mazao na jua yaani kuweka kivuli na gharama yake ni nafuu kulinganisha na greenhouse. Embu tujuze zaidi kuhusiana na hizo shed nets zako.
 
Na pia mazao kama nyanya, hoho, na matango hayahitaji maji mengi ndiyo sababu ni mahsusi kwenye gh hivyo msimu wa mvua hasara ya aliye lima open na shed nets ni sawasawa cos shed nets haizuii mvua.tuelimishe zaidi.
 
Mvua inayoingia kwenye shadenet house ni kidogo sana na hat hivyo Mvua haijawahi kuwa ni tatizo kwenye mazao bali, mvua nyingi kupita kiasi ndio huleta matatizo. Kingine ktk kucontrol maji mengi huwekwa plastic mulch kuhakikisha kiwango cha maji kinachokwenda kwenye mmea ni kile kinachotakiwa na unyevu unahifadhiwa vilivyo. Kwa hali ya hewa ya ukanda wa pwani Shade net zimekua more effective na gharama nafuu kwakua hali ya hewa haiitaji tena kuweka mfumo wa kupooza ambao huongeza gharama za uendeshaji.
Shadenet zinazotumika ni 75% shade factor ambazo lengo lake kubwa ni kupunguza Utraviolet light kwa 75% na kuruhusu mwanga kwa 25% only
Advantages

  • Helps in cultivation of flower plants, foliage plants, medicinal and aromatic plants, vegetables & spices.
  • Used for raising nurseries of fruits and vegetable.
  • Helps to enhance yield during summer season.
  • Protection against pest attack.
  • Protects crops from natural weather disturbances such as wind, rain, hail, frost, snow, bird and insects.
  • Used in production of graft saplings and reducing its mortality during hot summer days.
  • Used for hardening tissue culture plants.
  • Helps in quality drying of various agro products.
  • Helps in creating favourable micro environment for production of Vermi compost.

Application of Shadenets

  • Nursery propagation, floriculture, indoor plants, vegetables, tea, coffee, spices.
  • Hardening of plants.
  • Cattle shed, Fish Pond, Poultry Farming etc
  • Drying of various Agro products
  • Acts as a wind breaker
  • Greenhouse, terrace gardening & fencing
  • Used as safety nets for building repairs & constructions
  • Vermi compost unit
Type of Shadenets

  • Presently shadenets are available in different colours i.e. white, black, red, blue, yellow and green and in combinations:

  • Green x Black - cut off un-wanted U.V rays and gives aesthetic look. Used in grape for providing shade and helps in drying.
  • Black x Black - it absorbs and radiates heat inside the shadenet house. Used in nursery raising.
  • White x Black - diffuses the light inside the shadenet house. Mainly used for flowers such as Gerbera, Anthurium etc.
  • Green x Green - enhance the process of photosynthesis in plants resulting better foliage in ornamental plants.
 
Shida yangu in shed nets. Wapi naweza kuzipata name being zao

being=bei.
atuelimishe hapa sheets zinakua juu tu na pembeni ni net au?
Pia tsh3200,000/=ni bei nafuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…