Lowasa Alichafuka Wapi Mpaka Asafishwe?


Mkuu wa heshima mbele unantisha!!!
Angalia usifanye huyu Jamaa akakimbia humu jamvini.Inaonesha unamjua kwa karibu pamoja na Majina yake mengi atumiayo humu ndani.
Taabu ninayopata na huyu jamaa ni kuwa kila akianzisha topic hukimbia na kuwaachia watu wengine wachangie.!!
 

Du ama kweli mafisadi wamesambaza mihela. Huyu mpambe wa Lowassa sijui kapewa ngapi!!Labda ni kipofu haoni huo uchafu.
 
Nafikiri wanaomtuma huyu jamaa hapa JF wamepigwa bao. Natumaini hawamlipi maana kama wanamlipa...he's doing a very poor job...Anti whatever you may wish to call yourself...tafuta fani nyingine labda kuimba ngonjera..hii ya ku spin kaka toka jana nakuambia huiwezi.
 

Kama ile ya Dr. Slaa na umbea...
 
Taabu ninayopata na huyu jamaa ni kuwa kila akianzisha topic hukimbia na kuwaachia watu wengine wachangie.!!

Mkuu yupo sana, huwa ananzisha halafu anaanza kujibu kwa hoja tofauti, zingine anajitukana mwenyewe, zingine anashambulia wengine, lakini yupo tena sana wewe kumuoni huyu?

Hana cha upambe wala kutumwa na mtu yoyote, nafsi yake huwa inasikia raha sana kwa mambo kama haya, anachotaka ni attention lakini anajua kuwa hawezi kui-maintani kwa jina moja, ndio maana ana leta hizi nyepesi nyepesi!
 




Ngugu yangu naona sasa umewachoka watanzania, kama huna chakuandika kaa kimya unatukera bwana, wewe mtoto wa fisadi nini? kama huna point ya kuchangia kaa kimya
 
Jamani wajinga wajinga kama hawa(Antsadism) mimi naomba wafukuzwe humu ndani maana kitu anachozungumza yeye kipo wazi kwenye ripoti ya Mh. Mwakyembe
Nanukuu `Uteuzi wa mwisho wa Richmond Development Company LLC kuwa mkandarasi kufanywa na waziri Mkuu mwenyewe Juni 21 mwaka 2006
`Uamuzi wa serikali kuzuia Tanesco isivunje mkataba na kampuni hiyo licha ya sababu zote kisheria kuwepo ni baadhi tu ya viashiria vya nguvu kubwa iliyo juu ya Wizara ya Nishati na Madini kutumika katika suala hili,na kamati teule kutokana na ushahidi wa kimaandishi,kimazingira na mdomo,inaona nguvu hiyo kuwa ni Waziri Mkuu.....
 

Kazi ipo mkuu!
 

Weee Rich Rwassa tuondolee bangi zako.
 
LOWASA ALICHAFUKA WAPI WAPI MPAKA ASAFISHWE?

..................

Kwa hiyo, ni uzushi uliovuka mpaka na pia ni uongo mkubwa kudai eti Lowassa anasafishwa wakati hajachafuka chochote.

Kuandika ni kipaji. Usiigize unayoyaona humu. Andika kwa ufahamu wako badala ya kuiga ya wengine.

Hatuhitaji kujadili uozo wa Lowasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…