Mwacheni achukue fomu ila ninashindwa ataongoza bunge la aina gani. Najua ataamua kuendesha bunge kwa kulipiza kisasi na kuwaadhibu wabaya wake lakini wabaya wake ni Watanzania wapenda haki. Nina imani ataishia kujichakachua mwenyewe.
Imani yangu ni kuwa hawezi kufanya lolote kwani bunge hawezi kuliendesha kama anavyowafanya Wamasai huko Monduli. Atashangaa jinsi atakavyokwama mapema.
Hata Six sioni kama ana lolote la maana akirudi bungeni maana jinsi alivyohitimisha Richmond alitauacha hoi. Alijifanya mpiganaji hatimaye akishia kula matapishi yake.