Lowassa aliyekataliwa akimnadi Sioi atakubalika na Mzimu wake wa Richmond kwenye Urais?

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Ni wiki mbili sasa tangu Mbunge wa Monduli atawanye ubwabwa na Nyama lundo kwa wale anaowasema kuwa ni Rafiki wake, au Mashabiki wake, wakiwemo wenye viti wa mikoa na wilaya, hata baadhi ya mawaziri, na akaamua kutoa yaliyo moyoni, kwa kujinadi kuwa ni Rais au Mngombea Urais mtarajiwa, bila kupitishwa na vikao vyovyote vya chama. Wageni hawa ambo walikuwa wakila na kunywa mvinyo mkali pamoja na nyama choma, walifurahi sana kualikwa katika hafla hiyo ya mwaka mpya.

Pamoja na sherehe hii kali ambayo haijawahi kutokea katika mkoa huo, ya kwamba mtu binafsi anaweza kuita watu wengi wakashiriki kusherekea mwaka mpya huku wakiacha familia zao kibindoni. Si miugiza kwamba Je, walioenda huko ni watetezi wakweli wa wanyonge au ni washabiki wachumia tumbo.

Nilikuwa nikijiuliza ni vipi itakuwaje huyu mtuhumiwa aliyeshindikana kushitakiwa kwa kuhusika na dili la Richmond ambalo mpaka sasa bado ni mzigo wa misumari kwani kila kukicha TANESCO hutoongezea gharama kwa kuwa waliingizwa mkenge na wataka nchi, leo hii umeme imekuwa sitarehe ya kwanza. Huyu huyu alikataliwa kwao akiwa anamnadi Mbunge ambaye anamuoa mwanae (Ndg Sioii) mbali na ccm kuamia yote Arusha lakini waliaangukia pua, wapi ushwawishi wake, maana alisema anakuja kumaliza kila kitu na kiti kitarudi mikononi mwa ccm, hivi mtu anakataliwa kwao, bado watanzania wapo wanafurahia ubwabwa na mamilioni anayepewa na marafiki wake, ambayo hayalipiwi kodi wala hayajulikani yanatoka kwa nani.

Tunataka kupeleka Mtu ikulu Mahali pa Takatifu au Mahali patakwa vitu.

Soma
 
Ya Zitto ilikuwa chamtoto; ngoma ya Lowassa ni ya ki-utu uzima -- ni mpaka asubuhi.
 
Nitamkubari kama atapelekwa Mahakamani na kutoa ushahidi wa kutosha kuwa hausiki katika dili la Richmond na vielelezo visambazwe Tanzania nzima , hapo tutaona kuwa siye anayetuumiza bali ni sera za ccm tu, baada ya kukosa kutuletea maisha bora kwa kila mtanzania.
 
Mauaji ya wakulima yanayofanywa na wamasai yatakuwa mwiba kwake. Hata hivyo tumwache ajifurahishe yeye na washirika wake kwa kumuita/kujiita rais, rais, rais.....
 
Huyu jamaa hatufai,lkn tusiseme sana tukawashtua CCM wacha wamsimamishe.....kila nikifikiria mgogoro uliopo CDM roho inaniuma lkn baadae nafarijika nikijua kuwa kuna limgogoro linakuja CCM na hii itakuwa zaidi ya tufani siku mh Lowasa atakapotupwa nje asigombee urais kupitia huko,najua hawezi kukubali lkn pia hata akipitishwa kuna ambao nao hawawezi kukubali basi hapo ndio ngoma inogile..........
 
Poyoyo!! pesa ni kilakitu katika dunia hii hasa mataifa masikini, ccm haina ubavu kumtosa Lowassa.
 
Najiuliza maswali machache, na cpati majibu! Hivi nauli na posho za wenyeviti nchi mzima kwenda Monduli alitoa nani? Ukaaji Wao huko kwa siku walizokuwepo uligharamiwa na nani? Vilivyoliwa na kunywewa siku walizokuwepo huko viligharamiwa na nani? Kama yeye ndiye aliyetoa fedha zote hizo mfukoni kwake, zinatoka wapi? Naogopa kuendelea kumshabikia maana lazima zirudi, itakuaje?

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
Nyie ongeeni yote lakini Lowassa ndiye Rais ajaye. Tutampa kura za kutosha.
 
post yako imekaa kiwivuwivu wa kike tu
hakuna mantiki
hakuna hoja
hakuna jipya
kuna majungu
kuna umbea
kuna wivu
kuna roho mbaya

Ni wiki mbili sasa tangu Mbunge wa Monduli atawanye ubwabwa na Nyama lundo kwa wale anaowasema kuwa ni Rafiki wake, au Mashabiki wake, wakiwemo wenye viti wa mikoa na wilaya, hata baadhi ya mawaziri, na akaamua kutoa yaliyo moyoni, kwa kujinadi kuwa ni Rais au Mngombea Urais mtarajiwa, bila kupitishwa na vikao vyovyote vya chama. Wageni hawa ambo walikuwa wakila na kunywa mvinyo mkali pamoja na nyama choma, walifurahi sana kualikwa katika hafla hiyo ya mwaka mpya.

Pamoja na sherehe hii kali ambayo haijawahi kutokea katika mkoa huo, ya kwamba mtu binafsi anaweza kuita watu wengi wakashiriki kusherekea mwaka mpya huku wakiacha familia zao kibindoni. Si miugiza kwamba Je, walioenda huko ni watetezi wakweli wa wanyonge au ni washabiki wachumia tumbo.

Nilikuwa nikijiuliza ni vipi itakuwaje huyu mtuhumiwa aliyeshindikana kushitakiwa kwa kuhusika na dili la Richmond ambalo mpaka sasa bado ni mzigo wa misumari kwani kila kukicha TANESCO hutoongezea gharama kwa kuwa waliingizwa mkenge na wataka nchi, leo hii umeme imekuwa sitarehe ya kwanza. Huyu huyu alikataliwa kwao akiwa anamnadi Mbunge ambaye anamuoa mwanae (Ndg Sioii) mbali na ccm kuamia yote Arusha lakini waliaangukia pua, wapi ushwawishi wake, maana alisema anakuja kumaliza kila kitu na kiti kitarudi mikononi mwa ccm, hivi mtu anakataliwa kwao, bado watanzania wapo wanafurahia ubwabwa na mamilioni anayepewa na marafiki wake, ambayo hayalipiwi kodi wala hayajulikani yanatoka kwa nani.

Tunataka kupeleka Mtu ikulu Mahali pa Takatifu au Mahali patakwa vitu.
 
mkuu unapoteza muda wako bure kupiga porojo, haya kajipumzishe na wewe maana umepost na tumechangia
 
Back
Top Bottom