Lowassa amenifanya nikuchukie Diamond Platnumz

nyuli

Senior Member
Joined
Sep 7, 2012
Posts
128
Reaction score
95
Kati ya mashabiki waliokuwa wakikupigania huku mtaani Ni mm!

Kati ya mashabiki waliokuwa wakiperuzi page zako za facebook,instagram na tweeter kila saa Ni Mimi!

Kati ya shabiki ambaye nili kuwa nikiwachukia wabaya wako tena labda zaidi ya ulivyokuwa uliwachukia wewe Ni Mimi!

Kila nilipokua nikisikiliza habari zinazo kuhusu nilikua napata mvuto WA ajabu kuzisikiliza!

Hadi huku mtaani walikua wananitania eti mm Ni msemaji WA diamond!

Hata hapa jamii forums nilikua nakutetea Sana katika post zilizo kua zinakuponda,lakini dah kwa sasa naona bora Tu wakuponde!

Sababu Kuna jambo ambalo umelifanya yaani NATURALLY nimejikuta naanza kutovutiwa na wewe,sina stimu tena yaani najikuta Tu sivutiwi na staffs zako sio Kama napenda ila najikuta Tu.

Mfano nina Kama mwezi sasa sijui ishu zako maana nimeacha kukufatilia;kila nikitaka kufanya hivyo najickia hivyoo Tu!

Yaani hii ishu inatokea Tu automatic!


Sababu kubwa ya Mimi kuingiwa na hali hii Ni pale nilipo ona Kama msanii wangu nayekuthamini umeshindwa kujali hisia zangu za kisiasa.

Mi nadhani Kama ungekua unajua kuwa ilikupasa hata Kama unafanya kazi za chama flani nadhani ilikua poa ungezifanya Kama kazi lakini kitendo cha kuanza kujihuaisha na ushabiki WA kisiasa kwa kuanza kuuponda upande flani WA siasa bila kujali hisia za mashabiki zako tena wale WA damu umekosea mkuu.

Hisia zako za kichama ungebaki nazo moyoni mwako;kumbuka wewe Ni star mkubwa hapa nchini epuka kutengeneza confront za kihisia za mashabiki zako.

Kama management. Yako haikuliona Hilo mi nadhani hakukuwa na ulazima WA wewe kuanza kukandia upande flani kwa kejeli.


Una haki kuwa na chama ukipendacho lakini ungetumia busara katika kuwasilisha hisia zako hizo mbele ya uma.


Ukweli umenikwaza naamini hata wengine walio Kama Mimi watakua wamekwazika poa!


Epuka kuwauwa mashabiki zako kwa sababu ambazo zingekwepeka!


Sijajisikia poa!Isn't the same again.

LOWASA mabadiliko mabadiliko LOWASA!

CIAO!!!
 
Kuna msanii nilikua namkubali balaa haya mambo ya siasa yamenifanya anitoke ka ushuzi wa ngomani yani siku zile tu ka post. I think ushabiki wangu kwake hautakuwa Sawa tena aisee. Mi humkubali MTU Mara elfu zaidi kama tuna share common interests. Kama hazi match ndo baaas tena
 

Mpaka huku siasa napo, napita tuuu
 
Nadhani mpaka sasa utakuwa ushajielewa we ni shabiki mandazi... Na ndio tatizo kubwa la wengi wanaounga mkono Ukawa, """wanamawazo ya kibinafsi"" yani unapopakubali wewe na mtu flani apakubali la sivyo unamuona kama hajielewi hivi na amekosea sana...

Unaweza kutazama hata wasanii wanapopost masuala ya kisiasa, ukipost upo Ccm wa ukawa wanaanza kushambulia matusi, LAKINI ukipost upo ukawa mashabiki wa CCM hakuna anaekushambulia na Matusi japokuwa wapo wengi wa kutosha tu!!!

Mkuu WCB ni Crew kubwa sana, na habari za diamond kutozipata ni kujifungia ndani kutwa nzima usiingie kwenye social media, maana kuanzia mtaani, magazetini, mitandaoni kila kona CHIBUUUUUUUUUUUUUUUUUUU
 

Watu wa ukawa wana msongo wa mawazo ndio maana wanaota mabadiliko ambayo hayapo... We mtu anaamini eti lowassa akiingia Tanzania hakutakuwa na maskini sasa hizo akili au mafuta ya taa!
 

Ulikua huna haja ya kuniita sabiki maandazi!Lakini ucjari labda ndo kiwango chako cha utoaji hoja kilipo fikia.

Ulikua Ni ushauri Tu,sasa Kama mtu unaambiwa facts unakimbilia kuwaita watu maandazi;pole Sana WCB
 
Watu wa ukawa wana msongo wa mawazo ndio maana wanaota mabadiliko ambayo hayapo... We mtu anaamini eti lowassa akiingia Tanzania hakutakuwa na maskini sasa hizo akili au mafuta ya taa!


Sasa na wewe umekurupuka huko kuja kuropoka!sasa nani kaongelea mambo ya utajiri na umaskini hapa.

Unajua Mara nyingine Kama hujaelewa thread inadhima gani bora ukae kimya kuliko kuanza kuvamia thread za watu na kuandika un-related isues!
 
Kwani umelipa kiingilio shs. ngapi tukurudishi mpaka umnyime uhuru kipenzi cha watz wa kufanya kile anachoamini nisahihi kuwa mvumilivu siasa sio uadui
 
Sasa atajali hisia za wangapi? Ajali hisia za Zari, Tiffah, Esma, Mama na wewe piaaa...Hebu mpumzisheni mwana wa mwenzenu.....khaaa

Halafu ungeanza kuchukia ndugu zako woote wanaoshabikia CCM...

#Diamond ulipo nipo, you ll never walk alone...
 

Hahahahah Divabeyonce mambo.

Uchaguzi huu umetufanya wengi tuwe psychological victims .

Hawa wasanii hawa shabaash!,.
 
Last edited by a moderator:
Elimu ina umuhimu sana jaman, hasa kwa hawa wanamziki wetu....Elimu hakuna kabisa kichwani.

Ndo maana Nigeria wamepiga sana hatua, 80% ya wanamziki wakali wana degree zao....bongo wenye degree hata watano cjui km wanafika, Nawajua ROMA na Nikki wa II tu...
 

Hebu nitajie wasanii watano wa Nigeria walio 'hot' wenye degree, by the way Roma hana degree
 
1. Tiwa savage
2. Davido
3. Dr. Sid
4. Yemi Alade
5. Orezi

Ukitaka nkutajie na wengine nambie...

ROMA kasoma mlimani Computer Science....fatilia mkuu, Refer mathematics ''..me nmesoma PCM sio PCB...'' kende
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…