Ndugu yetu, mwenzetu Bwana Lowassa ametawazwa rami kuwa kiongozi wa kimila wa jamaa zetu Wamasai.
Kusimikwa huko kutampa nafasi ya kufanya ziara Arusha, Arumeru, Monduli, Morogoro, Usangu na kadhalika ili kujitambulisha rasmi.
Shirika la Taifa la Habari Tanzania [TBC] lilitumia takriban dakika 2 na nusu nzima kutangaza habari hizi.
Tunategemea pia na wabunge wa Kihaya, Kichagga, Kipemba, Kimakonde, Kiluguru, Kimeru, Kipare, Kigogo, Kikiha, Kinyamwezi, Kisukuma, Kinyakyusa, Kihehe, Kingoni na kadhalika watakaochaguliwa kuwa viongozi wa kimila wa makabila yao nao watapewa fursa sawa na mwenzetu Lowassa mara muda wao wa kusimikwa utakapowadia!
WAKATI huo huo Bwana Mkubwa Yusufu Makamba anasema kwamba CCM hailei wala haiwafugi MAFISADI. Swali ambalo Watanzania wengi wamejiuliza pamoja na ngonjera za kufuata mkondo wa sheria ni kuwa vipi kama polisi ni wa CCM, Mahakama ni za CCM, TAKUKURU ni ya CCM na TBC ni ya CCM na kadhalika na kadhalika huo mkondo wa sheria utatoka wapi.
Wanachokiomba wao ni kwamba Kamanda Mkuu wa Polisi ateuliwe na Bunge, Jaji Mkuu ateuliwe na Bunge, TBC iwe shirika h uru la habari linaloendeshwa kwa ruzuku ya serikali na kiongozi wake kuchaguliwa na Bunge na sio rais na mambo kama hayo ndio tutajua kweli CCM haiwafugi wala kuwalea MAFISADI!